Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
imempandisha kizimbani Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group and Company
Ltd, Mohamed Kiluwa (50) kwa tuhuma za kutoa rushwa ya Sh90 milioni kwa Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
Mshtakiwa huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa
Free Processing Zone alipandishwa kizimbani leo Agosti 2 mbele ya Hakimu mkazi
Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Huruma Shaidi na kusomewa shtaka moja la kujihusisha
na vitendo vya rushwa
Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Shaidi, Wakili wa
Serikali Mkuu kutoka Takukuru, Maghela Ndimbo amedai kuwa Julai 16 mwaka huu
kati ya saa sita mchana na saa nane, mshtakiwa huyo akiwa Mkurugenzi wa
kampuni hizo alitoa rushwa ya dola 40,000 sawa na Sh90 milioni fedha za
kitanzania kwa Waziri Lukuvi
Wakili Ndimbo alidai mshtakiwa huyo alitoa fedha hizo ili
asiwasilishe hati za umiliki wa kiwanja namba 57 Block B Kikongo na D Disunyura
vilivyopo eneo la viwanda Kibaha mkoani Pwani.
Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana hadi kesi itakapotajwa tena
Agosti 15
Apandishwa kizimbani kwa kujaribu kumhonga Sh90 milioni Waziri Lukuvi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment