Watu wawili akiwamo mwanafunzi wa Sekondari ya Mugumu Kurwa
Daniel (19) na raia wa kawaida Paulo Marwa (30) wamefikishwa mbele ya Hakimu
Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Serengeti mkoa Mara wakidaiwa kuiba pikipiki
Mwendesha mashtaka wa Polisi Renatus Zakeo ameiambia
mahakama kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Julai 27 mwaka huu
Alikuwa akiwasomea mashtaka hayo leo Agosti 2 mbele ya
Hakimu wa mahakama hiyo Ismail Ngaile
Mwanafunzi Daniel yeye alikamatwa leo Agosti 2 akiwa shule,
akasomewa mashtaka akiwa amevaa sare zake za shule na mkononi akiwa meshika
madaftari yake
Amesema waliiba pikipiki aina ya Toyo mali ya Benjamin
Kiboge yenye thamani ya Sh2 milioni
Washtakiwa wote wamekana mashitaka na wamepelekwa mahabusu
hadi Agosti 10 mwaka huu itakapotajwa tena
Mwanafunzi apandishwa kizimbani akidaiwa kuiba bodaboda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment