Kutokana na upungufu wa ukwasi Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
imechukua usimamizi wa Benki M Tanzania kuanzia leo, Agosti 2.
Akiongea na waandishi wa habari, Gavana wa BoT Profesa
Frolens Luoga amesema uamuzi huo umetokana na benki hiyo kuwa na ukwasi mdogo
kuliko matakwa ya Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006
"Upungufu wa ukwasi ulioshuhudiwa katika benki hii
unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa
Benki M kunahatarisha amana za wateja wake hivyo kwa siku 90 kuanzia sasa benki
hiyo haitatoa huduma," amesema Profesa Luoga
Ameongeza kuwa BoT imeisimamisha bodi ya wakurugenzi na
uongozi wa Benki M na mamlaka hiyo ya juu ya usimamizi wa sekta ya fedha
itakuwa ikifanya tathimini ya kusaidia kupata ufumbuzi wa suala hilo
Benki M inakuwa ya 10 kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa
BoT ndani ya miaka miwili
Benki sita kati ya zilizowekwa chini ya uangalizi zimefutiwa
leseni za biashara na tatu zikiunganishwa na nyingine
Kati ya zilizofutiwa leseni ni Benki ya FBME na Benki ya Wananchi
Mbinga wakati Twiga Bancorp na Benki ya Wanawake (TWB) zikiunganishwa na Benki
ya Posta na Benki ya Wananchi Tandahimba ikiungana na CRDB
Benki M yawekwa chini ya usimamizi wa BoT
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment