Watu wanne wamefariki dunia watatu wakiwa ni wa familia
katika ajali iliyohusisha gari na pikipiki
Akizunguma na wanahabari leo Agosti 2, Kamanda wa Polisi
mkoani Dodoma Gilles Muroto, amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo
wilayani Bahi, Dodoma kwenye barabara kuu ya Singida-Dodoma
Waliofariki ni watoto Yusra Salum (5), Karialino Hamis (2),
Hussein Hamisi (miezi miwili) na Mfaume Hamis (30) ambaye alikuwa dereva wa
bodaboda
Kamanda Muroto amesema mwendesha pikipiki huyo alikuwa
amewapakia watoto watatu na mama yao na aliingia barabarani ghafla na pikipiki
hiyo iligongwa na basi la kampuni ya Satco
Muroto ameeleza kuwa basi hilo lilikuwa likitokea Mwanza
kuelekea jijini Dar es salaam
“Kwenye hiyo pikipiki walikuwa wamepanda jumla ya watu
watano, watoto watatu na mama yao dereva amefariki dunia papo hapo na watoto
watatu mama huyo na mama mwenyewe naye ni majeruhi hospitali,”amesema
Ajalia yaua watoto watatu wa familia moja
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment