SERIKALI Wilayani Kahama mkoani Shinyanga imesema
itawachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani
wanaowatumia watoto wadogo chini ya miaka kumi na nane katika shughuli za uchimbaji
wa madini
Watoto wadogo wamekuwa wakitumiwa na wachimbaji wadogo wa
madini hasa katika shughuli za kuchota maji na kusomba mawe ya dhahabu na
kupeleka katika maeneo ya uchenjuaji wa madini, hali ambayo inawafanya watoto
hao kukosa masomo
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, alisema jana
lengo la serikali ni kuona kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anakwenda shuleni
kupata elimu ambayo itakuwa mkombozi kwa maisha yake ya baadae
Alisema asilimia kubwa ya wananchi wilayani hapa
wanajishughulisha na uchimbaji wa madini, kilimo na ufugaji, hali hiyo ndio
inayopelekea watoto kukosa masomo na kuinguia katika shughuli hizo
"Nataka kuona kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule
anakwenda shuleni mara moja na sio kwenda katika shughuli za uchimbaji wa
madini, kilimo au kwenda kuchunga mifugo ya baba yake,” alisema
Macha aliongeza: “Tunataka kuona wazazi wanakuwa mstari wa
mbele kulitokomeza hili la watoto kutumikishwa na wachimbaji wadogo na kwahili
lazima tushirikiane na wazazi, viongozi wa wachimbaji na wachimbaji wenyewe
Alisema mambo mengi yanatokana na wazazi kuwa na mwamko
mdogo wa elimu hasa wale waliko pembezoni mwa mji na kwamba serikali itaendelea
uwapatia elimu ili watambue umuhimu wa elimu kwa watoto wao
Katika hatua nyingine Macha alisema kila mfanyabiashara ambaye
anafanya biashara inayomwingizia kipato anatakiwa kulipa kodi kwa wakati
sambamba na kutumia vema mashine ya elektroniki (EFD) ili kupunguza migogoro
yao na Mamkala ya Mapato (TRA
Alimtaka Meneja wa TRA mkoa Mkoa maalum wa kikodi Kahama,
Jacobo Mtamang'ombe, kutoa elimu juu ya matumizi ya EDF kwa wafanyabiashara
walioko pembezoni mwa mji
Wanaotumia Watoto Migodini Kukiona Cha moto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment