Wananchi wa kijiji cha Terrat wilayani Simanjiro
mkoani Manyara watakaokata miti, kutupa taka na kulishia mifugo kwenye chanzo
cha maji cha Mto Terrat watacharazwa viboko 70
Adhabu hiyo imetokana na wazee wa kimila wa jamii ya wamasai
kupitisha sheria baada ya kutokea uharibifu wa mazingira kwenye mto huo na
kusababisha maji kukauka
Mmoja wa wazee wa kimila wa eneo hilo, Leshule Lesindiya
akizungumza jana Alhamisi Agosti 16, 2018 amesema wamepitisha sheria hiyo kwa
mtu atakayekiuka maagizo hayo kwa lengo la kuhakikisha wanaendelea kutunza
mazingira ya eneo hilo
Amesema wanaishukuru Serikali kwa kuridhia utekelezaji wa
sheria hiyo ndogo ambayo kwa namna moja au nyingine itawasaidia wananchi wa
eneo hilo kuepuka uharibifu wa mazingira uliokuwa ukifanyika
"Awali ilionekana kama ni ubabe pindi mtu akipatiwa
haki yake ya msingi ya kuchapwa viboko 70 kwa kuharibu mazingira lakini sasa
wananchi wameeleweshwa na mtu akikosea anakubaliana na adhabu hiyo kwani si kwa
ajili ya kuonewa ni kosa lake mwenyewe,"amesema
Mwenyekiti wa kijiji cha Terrat, Godson Nduya amesema Mto
Terrat ni mto wa asili kwenye wilaya ya Simanjiro unaohudumia zaidi ya wananchi
wa vijiji saba
Nduya amesema vyanzo vya maji vilivyokuwa vinasaidia mto huo
kuwa na maji nyakati za kiangazi na masika ni miamba ya asili yenye chemchem
inayotiririsha maji kila wakati
Amebainisha kuwa uwepo wa maji kwa kipindi chote cha miaka
ya nyuma ni kutokana na kuwa na mimea asili ambayo kwa kiasi kikubwa ilisaidia
kutunza na kuhifadhi mto ila hivi sasa sehemu kubwa ya miti hiyo imekatwa
Mkazi wa kijiji hicho, Joseph Lengenyu amesema sheria hiyo
kwa namna moja au nyingine itachangia wananchi kuheshimu mazingira na kuyatunza
kwani bila kuchukuliwa hatua hakuna kitu kitafanyika
Wananchi Simanjiro kucharazwa viboko 70
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment