Lugola: Polisi wakamateni wanafunzi watoro


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ametoa wiki moja kwa polisi wilayani Bunda mkoani Mara kuwakamata wanafunzi watoro na wazazi wao.

 Pia, agizo hilo litawakumba watu waliowarubuni wanafunzi wa kike na kuwasababishia kukatisha masomo

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Mwibara ametoa kauli hiyo jana jioni Alhamisi Agosti 16, 2018 mkoani humo na kubainisha kuwa anasikitishwa na idadi kubwa ya wanafunzi walioacha shule wilayani humo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kurubuniwa na wanaume

Amesema  kiwango cha wanafunzi kuacha masomo kinazidi kuongezeka hivyo Serikali haiwezi kukaa kimya, lazima ifanye kitu kuhakikisha wanafunzi hao wanasoma ili waje kuwa viongozi wa nchi

“Mkuu wa Polisi hapa Bunda, nawapa wiki moja, mtumie elimu zenu za upelelezi mliofundishwa, wakamateni, wachunguzeni, wahojini ndugu,  jamaa, majirani mtawapata wote wanaowarubuni watoto hawa, halafu mushughulike nao,” amesema Lugola.
Lugola: Polisi wakamateni wanafunzi watoro Lugola: Polisi wakamateni wanafunzi watoro Reviewed by KUSAGANEWS on August 17, 2018 Rating: 5

No comments: