Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limezungumzia kutosafiri
kwa ndege yake mpya aina ya Boeing 787-7 Dreamliner, iliyoanza kazi mwishoni
mwa mwezi uliopita
Tangu ilipoanza safari zake Julai 29, ndege hiyo imekuwa
ikifanya safari kati ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza kila siku asubuhi
na jioni
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Ladislaus Matindi alisema
juzi kuwa, hakuna ndege yao ambayo imekwama mahali popote na hata Dreamliner
ambayo shirika limeisimamisha kwa makusudi kutokana na matakwa ya kiufundi
“Tunazo ndege nne, tatu aina ya Bombardier Q400 zinaruka na
kufanya safari zake kama kawaida, Dreamliner tumeisimamisha sisi wenyewe kwa
ajili ya matakwa ya kiufundi, kwa hiyo iko chini kuanzia jana (Agosti 14), leo
(Agosti 15) na kesho (Agosti 16),” alisema Matindi wakati akizungumza na kituo
cha televisheni cha Azam, juzi
Alisema nia ni kuangalia sehemu za marekebisho katika ndege
hiyo ikiwemo suala la WiFi ambayo inatakiwa kufanyiwa marekebisho madogo na
mambo mengine yanayohusiana na uendeshaji kwa kuwa safari zinazofanyika sasa ni
za majaribio na mafunzo kwa marubani
“Ndege ilisimamishwa ili kufanyia marekebisho ambayo
yanatakiwa katika uendeshaji. Hayo yanayosemekana siyo kweli na kesho (jana)
tutakuwa tumemaliza na tutaendelea na safari za Dreamliner,” alisema.
Awali, baadhi ya
taarifa zilisambaa mitandaoni zikidai ndege hiyo ilikuwa na matatizo
yaliyosababisha abiria waliotakiwa kusafiri nayo kukwama hadi wakatafutiwa
ndege nyingine
Matindi alisema ATCL walipanga kuwa matengenezo yangefanyika
baada ya wiki tatu, lakini mafundi waliomba yafanyike mapema kwa sababu
wanakaribia kuondoka, hivyo ikabidi shirika lifanye uamuzi wa ghafla
“Marekebisho yalifanywa baada ya kukamilika kwa safari moja
ya kutoka Mwanza kurudi Dar es Salaam, hivyo hakuna abiria yeyote aliyetelekezwa
wala kushushwa uwanja wa ndege kama inavyoelezwa,” alisema
Kwa upande wake, Mkuu wa Mawasiliano wa ATCL, Joseph Kagirwa
alisema abiria wote ambao walitakiwa kusafiri na Dreamliner kwa safari zao,
baadhi yao walisafirishwa na Bombardier na wengine walipandishwa katika ndege
za mashirika mengine
“Tulifanya mawasiliano na abiria wetu siku moja kabla, kila
mmoja alipigiwa simu kuelezwa dharura iliyojitokeza, hakuna mtu aliyetozwa
nauli zaidi na ofa zetu zinaendelea kama kawaida,” alisema Kagirwa
“Kesho Dreamliner inarejea katika safari zake kama kawaida
na ndege itakuwa imejaa.”
Baadhi ya wasafiri
ambao walitarajia kusafiri na ndege hiyo kutoka Kilimanjaro kwenda Dar es
Salaam juzi, walilazimika kukaa uwanjani kwa zaidi ya saa nane
Abiria waliozungumza na gazeti hili walilalamikia kutopewa
taarifa mapema juu ya ndege hiyo iliyotakiwa kuondoka uwanjani hapo saa sita
mchana, lakini haikufika
“Tuko uwanjani hapa toka saa nne na tulitakiwa tuondoke
kuelekea Dar es Salaam majira ya saa sita mchana, lakini hadi sasa bado
hatujaondoka,” alisema mmoja wa abiria ambaye hakutaka jina lake liandikwe
gazetini
Baadaye abiria huyo alisema waliondoka kwa makundi kwa
kutumia ndege za mashirika mengine
Abiria huyo alisema kundi la kwanza liliondoka uwanjani hapo
saa 12 jioni na la mwisho liliondoka saa mbili usiku
“Baadhi ya abiria wameshasafiri kwa kutumia ndege za kampuni
nyingine, lakini abiria 15 kati ya 50 tuliotarajia kusafiri kwa ndege hiyo bado
tupo uwanjani, hatujui hatima yetu,” alisema abiria huyo kabla ya baadaye
kusema walifanikiwa kuondoka saa mbili usiku
Sababu za Dreamliner kutoonekana Mawinguni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment