TAARIFA ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, mwaka jana, inatarajia kuchambuliwa
kwenye vikao vya Kamati za Bunge zinavyotarajia kuanza keshokutwa
Vikao hivyo vinatarajia kufanyika jijini Dodoma kabla ya
kuanza kwa mkutano wa 12 wa Bunge uliopangwa kuanza Septemba 4, baada ya Spika
wa Bunge, Job Ndugai, kuziita Kamati hizo kuanza shughuli zake
Taarifa hiyo ilieleza kuwa taarifa ya CAG itachambuliwa na
kamati zinazosimamia matumizi ya fedha za umma ambazo ni Kamati ya Hesabu za
Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC
Aidha, taarifa hiyo ilitaja shughuli zilizopangwa
kutekelezwa na kamati ni uchambuzi wa miswada mitano ya sheria ambayo
itajadiliwa na kamati nne zilizopelekewa miswada hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya
84 (1
“Kamati ya utawala na serikali za mitaa itachambua na kujadili
muswada wa sheria ya ‘Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi wa
mwaka 2018,’’ ilisema
Pia ilisema kamati ya Katiba na Sheria itachambua na
kujadili miswada miwili ambayo ni ‘Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
mbalimbali (na.2) wa mwaka 2018
Taarifa hiyo iliutaja muswada wa pili kuwa ni wa sheria ya
Marekebisho ya sheria mbalimbali (na.3) wa mwaka 2018
“Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii itachambua na
kujadili ‘Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalam ya Walimu Tanzania wa mwaka
2018’,” ilieleza
Kadhalika, Kamati ya Bajeti itachambua na kujadili ‘Musada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi wa mwaka 2018,” ilisema
Pia taarifa hiyo ilisema Kamati tisa za sekta, Kamati ya
bajeti na Kamati ya Masuala ya Ukimwi, zitachambua taarifa za taasisi na wizara
kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali.
Taarifa hiyo ilisema kuwa kamati ya Bunge ya sheria ndogo
itachambua sheria ndogo 121 zilizowasilishwa bungeni Aprili 9, mwaka huu,
wakati wa mkutano wa 11 wa Bunge
“Madhumuni ni kutekeleza majukumu yake yaliyoainishwa katika
kifungu cha 11 cha nyongeza ya nane ya kanuni za Bunge,” ilisema taarifa hiyo
Pia kamati ya uwekezaji wa miradi ya umma (PIC) itachambua
taarifa ya uwekezaji wa taasisi, mashirika 13 kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha
nyongeza ya nane ya Kanuni za Bunge
Wabunge kujadili ripoti ya CAG
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment