Idadi ya magari yaliyoteketea kwa moto katika kituo cha
forodha Rusumo Wilaya ya Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda,
imeongezeka na kufikia saba na trekta moja huku utingo wa moja ya gari hayo
akipelekwa hospitalini baada ya kujeruhiwa
Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mntenjele
amesema tukio limetokea leo Agosti 19, 2018
Kanali Mtenjele amesema utingo wa gari lililokuwa limebeba
petroli alibahatika kuruka na kuumia na amepelekwa Hospitali ya Nyamiaga kwa
matibabu, huku eneo la tukio likiwa limetanda taharuki kutokana na ukosefu wa
gari la zimamoto
"Tumewasiliana na viongozi wenzetu wa nchi jirani
ya Rwanda wameahidi kutuma helikopta ya kuzima moto na kuokoa mali za wananchi
na maisha yao," amesema
Amesema kukosekana kwa gari la zimamoto wilayani Ngara hasa
kata hiyo ya Rusumo ni changamoto kubwa katika kuokoa maisha ya wananchi na
mali zao
Wakala wa forodha kituo cha Rusumo, Abdul Shakuru alisema
gari lililosabanisha ajali ni mali ya kampuni ya Lake Oil na magari mengine ni
ya kampuni ya Azam ambayo hufanya shughuli zake za kusafirisha
mizigo kutoka Tanzania kwenda Rwanda
Amesema takriban magari 60 yaliyokuwapo na kwamba, kwa siku
yanapita zaidi ya 80 mpaka 100 yanayosafirisha mizigo kwenda Rwanda na DRC
Kongo, huku mengine yakirejea Dar es Salaam
Shakuru amesema licha ya vituo vya forodha kufanya kazi saa
24 kwa Tanzania na Rwanda, changamoto upande wa Ngara hakuna maegesho ya
uhakika na tukio hili la kuteketea magari liinaweza kuwa sita kwa miaka mitatu
iliyopita.
Eneo palipotokea ajali hiyo ni umbali wa kilomita 40 kutoka
Rusumo hadi makao makuu ya Ngara na kilomita tatu kuingia kituo cha forodha
upande wa Rwanda, zikiwa ni kilomita 130 kutoka Rusumo kwenda Karagwe
ambako kuna gari la zimamoto
Utingo ajeruhiwa, magari saba yakiteketea Rusumo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment