Viongozi wamiminika Muhimbili kumjulia hali Kigwangalla


Mawaziri mbalimbali wamefika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kumjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliyepata ajali leo asubuhi Jumamosi Agosti 4, 2018

Dk Kigwangalla amepata ajali eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini

Awali,  waziri huyo alipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu na kuhamishiwa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa helkopta na kisha Muhimbili

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alikuwa wa kwanza kufika hospitalini hapo na kufuatiwa na naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Dk Ashatu Kijaji na naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni aliwasili na  viongozi mbalimbali wizara hiyo na ya Maliasili na Utalii.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya na mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru pamoja na jopo  la madaktari walimpokea Dk Kigwangalla katika kitengo cha magonjwa ya dharura Muhimbili

Ndugu, jamaa na marafiki pia walifika hospitalini hapo kumjulia hali waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa Nzega Vijijini

Viongozi wamiminika Muhimbili kumjulia hali Kigwangalla Viongozi wamiminika Muhimbili kumjulia hali Kigwangalla Reviewed by KUSAGANEWS on August 04, 2018 Rating: 5

No comments: