Dar es Salaam. Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji
Peter Msigwa amesema katika msafara wa mamba, kenge wapo, akifananisha msemo
huo wa wanachama wa vyama vya upinzani wanaohamia CCM
Amesema katika harakati za kuleta mabadiliko si jambo la
ajabu wakatokea wasaliti, kubainisha kuwa wasaliti hao ni waliokuwa viongozi na
wanachama wa Chadema na vyama vingine vya upinzani waliohamia chama tawala
Mchungaji Msigwa ametoa kauli hiyo leo jioni Jumapili Agosti
5, 2018 katika kipindi cha Siasa za Kanda kinachorushwa na kituo cha
televisheni cha KTN cha nchini Kenya
Mada kuu katika kipindi hicho ilikuwa ni kujadili hali ya
siasa za upinzani barani Afrika huku wachangiaji wa mada hiyo wakiunganishwa
kutoka Zambia, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), Zimbabwe, Kenya, Uganda na
Tanzania
Mchungaji Msigwa ametoa kauli hiyo baada ya kuulizwa na
mtangazajii anaonaje hali ya Chadema katika kujiimarisha katikati ya mazingira
ya viongozi na wanachama wake kuhamia CCM
Katika ufafanuzi wake Mchungaji Msigwa amesema licha ya kuwa
kuhama chama ni haki ya msingi, wengi wanachukua uamuzi huo kwa kushawishiwa
kwa ahadi mbalimbali
“Kama wangekuwa wanachukuliwa na kufanya kazi ya chama mimi
sioni tatizo lakini wanaahidiwa nafasi za uongozi, hii si sawa kabisa. Hii
inaua mawazo pinzani,” amesema
mbunge huyo wa Iringa Mjini amekiri changamoto hiyo ya
wanachama kuhama haipo Tanzania pekee bali kwa vyama vingi vya upinzani barani
Afrika, kubainisha kuwa Chadema wanaongeza mbinu za kujenga imani na itikadi
kwa wanachama wao
Akichangia mada hiyo, Profesa Fulbert Namwanga raia wa Kenya
anayefundisha nchini Marekani amesema demokrasia katika nchi nyingi za Afrika
haijakomaa
“Demokrasi si pevu ina ufisadi mwingi, baadhi hawaelewi
maana ya demokrasia na hawaelewi maana ya upinzani wanauona kama uadui. Ni
kawaida wapinzani kununuliwa, ni jambo la kuhuzunisha sana,” amesema
Mchungaji Msigwa ataja siri ya Ukawa kuishinda CCM 2020
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment