Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Uchaguzi Mdogo wa
Ubunge katika majimbo matatu na wa udiwani katika kata mbili za Tanzania Bara
utakaofanyika Septemba 16, mwaka huu
Akitangaza uchaguzi huo mjini Dodoma leo Agosti 4 Makamu
Mwenyekiti wa NEC Jaji Mbarouk Salim Mbarouk amesema fomu za uwa wagombea wa Majimbo hayo zitatolewa kuanzia tarehe 13 hadi 20 Agosti mwaka
huu na uteuzi utafanyika tarehe 20 Agosti, 2018
Amesema kampeni zitaanza Agosti 21 na
kumalizika Septemba 15, mwaka huu
“Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha
Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge
katika Majimbo matatu”amesema Jaji Mbarouk
Ameyataja majimbo hayo kuwa ni Korogwe Vijijini, Mkoa wa
Tanga kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Stephen Hilary Ngonyani,
Jimbo la Ukonga Katika Mkoa wa Dar Es Salaam na Jimbo la Monduli katika Mkoa wa
Arusha
Alisema wabunge wa majimbo hayo mawili Mwita Mwikabe
Waitara na Julius Kalanga Laizer walijiuzulu uanachama CHADEM) na hivyo
kupoteza sifa za kuwa Wabunge
“Baada ya kupokea taarifa hizo na kwa mujibu wa vifungu vya
37 (1) (b) na 46 (2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi
inatoa taarifa kwa Umma kuwa majimbo matatu ya Korogwe Vijijini, Ukonga na
Monduli yapo wazi”, amesema
Katika hatua nyingine, Jaji Mbarouk amesema kwa kuzingatia
masharti ya vifungu vya 37(1)(b) (5) na 46 (2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,
Tume inatoa taarifa wa Umma kuhusu Ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo hayo
Ameongeza kuwa Tume pia inatoa taarifa kwa umma kuwa uteuzi,
Kampeni na uchaguzi wa Madiwani kwa Kata za Tindabuligi na Kisesa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu uliohirishwa hapo awali utafanyika sambamba na
ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa ubunge katika Majimbo hayo matatu
“Tume inachukua nafasi hii kuvikumbusha Vyama vya Siasa na
wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo na
Maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo wa Majimbo hayo matatu na
hizo Kata mbili” amesema
Uchaguzi huu mdogo wa majimbo matatu na kata mbili za
Tanzania Bara, unafuatia uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Buyungu
unaotarajiwa kufanya Agosti 12 pamoja na kata 37 za Tanzania Bara
Uchaguzi mdogo wa ubunge kufanyika Septemba 16
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment