Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi
maarufu Sugu leo Jumamosi Agosti 3, 2018 ametinga katika mkutano wa
hadhara na faili lenye orodha ya ahadi mbalimbali alizozitekeleza tangu mwaka
2015
Akizungumza leo jioni katika mkutano huo uliofanyika katika
stendi ya Tukuyu-Uyole mjini hapa, Sugu amesema ameamua kufanya hivyo baada ya
kuibuka maneno ya kumchafua kuwa hajafanya chochote tangu alipochaguliwa kuwa
mbunge
"Makamanda msishangae kuniona nimeshika faili mkononi.
Nipo hapa kwa ajili ya kuwaeleza mambo niliyoyafanya tangu mliponichagua
maana kuna watu wanazunguka mitaani kunichafua kuwa sijafanya kitu"
amesema Sugu
Amesema tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa
mbunge mwaka 2010 hadi sasa amefanikiwa kujenga madaraja zaidi ya 10
yanayounganisha jiji la Mbeya na Mbeya vijijini pamoja na kujenga maabara za
kompyuta kila shule ya kata na kusomesha watoto yatima zaidi ya 400
"Nimefanya vitu vingi lakini mimi sio mtu wa kiki
eti niwaite waandishi wa habari kwa kila kitu ninachokifanya kama
wapinzani wangu wanavyofanya,” amesema Sugu
Sugu atinga mkutanoni na faili, afunguka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment