Dk Kigwangalla awasili Muhimbili


Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amewasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi

Ndege iliyombeba waziri huyo imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 jioni, msafara kuondoka kuelekea Muhimbili

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya na mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru pamoja na jopo  la madaktari wamempokea Dk Kigwangalla katika  kitengo cha magonjwa ya dharura Muhimbili

Dk Kigwangalla amepata ajali leo Jumamosi Agosti 4, 2018 eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini

Awali,  waziri huyo alipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu na kuhamishiwa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa helkopta

Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba amefariki dunia

Dk Kigwangalla awasili Muhimbili Dk Kigwangalla awasili Muhimbili Reviewed by KUSAGANEWS on August 04, 2018 Rating: 5

No comments: