Serikali yaanza kuboresha Miundombinu ya Elimu kwa Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum


Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Tekolojia Mh William Olenasha amesema serikali ya awamu ya Tano inajitahidi kuboresha Elimu kwa nchi nzima ili kuboresha elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Mh Olenasha amesema hayo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kisasa iliyoko Chuo cha Patandi mkoani Arusha ambapo wanafunzi 600 watasoma katika Shule hiyo wengi wao wakiwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Hata hivyo amesema Kila wakati wanapojenga Shule na miundombinu ya elimu iwe Vyuoni au Shule za Msingi lazima majengo yawe rafiki kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum ili iwe rahisi kwa wao kuwa kama watu wengine.

“Hatutaki watengwe kwahiyo kama hatuwatengi kwenye jamii hatutaki vilevile watengwe wakiwa shuleni kwa hiyo Shule hii pamoja na kuwa kwa kiasi kikubwa itakuwa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum lakini watakuwepo wa kawaida kwasababu tunataka wachangayike”Alisema Olenasha

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo hicho cha Elimu maalum Patandi Jenasi Lenai amesema kuwa kukamilika kwa shule itasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum kusoma kama wanafunzi wengine wasio na mahitaji.

Amesema kuwa kujengwa kwa majengo hayo ni kwa ajili ya kuwachanganya pamoja wanafunzi wenye uhitaji na wasio na uhitaji ili kuwafanya wasijisikie kama wametengwa na jamii.

Naye Mhandisi mshauri wa mradi huo Bwana Israel Mahege amesema kuwa mradi huo wa sekondari tayari umekamili kwa asilimia 60 na wanasubiria pesa nyingine kwa ajili ya kumalizia.
Serikali yaanza kuboresha Miundombinu ya Elimu kwa Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum Serikali yaanza kuboresha Miundombinu ya Elimu kwa Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum Reviewed by KUSAGANEWS on August 01, 2018 Rating: 5

No comments: