Mbunge wa Malindi (CUF), Ally Saleh amedai Chama cha
Mapinduzi (CCM) kimehamishia nguvu visiwani Zanzibar kuwashawishi wanachama wa
vyama vya upinzani wajiunge nacho
Akizungumza Saleh amesema yeye ni miongoni mwa
wanaoshawishiwa kujiunga na chama hicho tawala
Kabla ya kuzungumza Saleh alitoa tuhuma hizo kupitia ukurasa
wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter huku CCM visiwani humo kikimjibu, kumtaka
kutoweweseka badala yake, atulie kushuhudia wimbi la wana CUF watakaokihama
chama hicho
Katika ukurasa wake huo, mbunge huyo aliandika alichoelezwa
na aliyemtambulisha kuwa ni mgeni (kutoka CCM) aliyekwenda nyumbani kwake
na jinsi alivyomjibu
Saleh: Kisa kuja kwangu?
Mgeni Sijatumwa, mimi
mwenyewe
Saleh Kitu gani?
Mgeni: Tunataka uje kujiunga CCM
Saleh: Shuka ngazi haraka na mlango wa nyumba yangu usiujue
Akifafanua zaidi alipozungumza Saleh amesema, “ni kweli
alikuja nyumbani kwangu, alipofika sikuwa nikimjua lakini alipoanza
kujitambulisha ndio nikamjua.”
“Mtu huyo ni wa hapa Zanzibar lakini kwa sasa sitamtaja
majina yake ila akibisha nitamtaja. Labda niseme tu kwamba, mimi sinunuliki,
nimezaliwa upinzani na sitarajii kwenda CCM.”
Amesema alimtaka kigogo huyo kutokurudia kumshawishi kwa
maelezo kuwa yeye si kama wengine wanaoshawishika
Akizungumza msemaji wa CCM- Zanzibar, Catherine Nao amemtaka
Saleh kumtaja mtu huyo aliyekwenda kumshawishi, “wanaokuja CCM wanakuja si kwa
ushawishi, wanakuja wao wenyewe kwa kuona mambo mazuri anayoyafanya.”
“Hakuna anayeshawishiwa, Rais Magufuli (John) yale
anayoyafanya ndio anawafanya wajiunge na CCM, lakini niseme tu, Septemba 15,
2018 tukiwa tunazindua kampeni za uwakilishi wa Jang’ombe, kuna wana CUF wengi
watajiunga na CCM, subirini mtaona.”
Mbunge CUF adai kushawishiwa kuhamia CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment