Rais John Magufuli ameeleza sababu za kumteua David Kafulila
kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe kuwa ni jinsi alivyopambana katika kashfa
ya akaunti ya Tegeta Escrow iliyohusu kampuni ya Independent Power Tanzania Ltd
(IPTL).
Rais ameyasema hayo leo Agosti Mosi wakati akiwaapisha
makatibu wakuu, manaibu katibu wakuu, makatibu tawala na wakuu wa mikoa
“Ndugu yetu Kafulila alipokuwa huko kwenye chama chake
alipigania suala la IPTL, nani anayeipenda IPTL tulivyofanyiziwa? Uwe CCM uwe
Chadema uwe CUF uwe huna chama, suala la IPTL halina chama,”
“Lakini alisimama akapingwa, akaitwa tumbili akaitwa
nani wala hajageuka kuwa tumbili ni huyu huyu. Huyu siyo mpianzani bali ni
mtekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi,” amesema Rais Magufuli
Amewataja baadhi ya viongozi wakiwamo makatibu tawala na
kusema lakini aliyekuwa mpinzani ni Kafulila peke yake, huku kwa wakuu wa
wilaya akisema wapo watatu na nusu
“Ukingalia ma-RAS, aliye cross chama ni mmoja tu, Kafulila,
katika 13 wote. Ukienda kwa Ma-DC wako 31, niliowakuta nafikiri ni watatu na
nusu walio cross vyama vingine. Kuna huyo wa Dodoma (Katambi) mjini, Longido,
kuna wa Nanyumbu nafikiri Machali na Bukombe ambaye ndiyo naita nusu (Nkumba)
ambaye alikaa CCM kule akahamia upinzani siku tatu akarudi huku,” amesema
Rais amesema lengo lake ni kujenga nchi yenye umoja, isiyo
na ubaguzi wa dini, kabila wala vyama na yuko tayari kuwashirikisha wote
wanaotaka kupeleka mbele nchi
Rais John Magufuli ataja sababu za kumteua Kafulila
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment