Jeshi la
Polisi limefungua jalada la uchunguzi dhidi ya kauli zilizotolewa na mbunge wa
Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe
Akizungumza
leo Jumatano Agosti Mosi, 2018 msemaji wa polisi, Barnabas Mwakalukwa amesema
kwa sasa uchunguzi unafanyika kuhusiana na tuhuma zinazomkabili mbunge huyo
ambaye pia ni kiongozi wa ACT
Mwakalukwa
ameeleza hayo ikiwa imepita siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani,
Kangi Lugola kumtaka kiongozi huyo kujisalimisha polisi kwa maelezo kuwa
ametoa kauli za uchochezi
Lugola amesema
Zitto ametoa kauli za uchochezi na kuwatukana viongozi wa Serikali wakati
akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Kilwa Kusini,
mkoani Lindi
Katika mkutano
huo Zitto alialikwa na mbunge wa jimbo hilo, Seleman Bungara maarufu Bwege
Mwakalukwa
amesema kufuatia agizo hilo la Lugola tayari wamefungua jadala kuchunguza jambo
hilo, kwamba uchunguzi ukikamilika na iwapo itaonekana mbunge huyo anahitajika,
watamuita polisi
Amesema polisi
wanafanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria, kwamba Zitto akihitajika
ataripoti kwa kamanda wa polisi mkoani Lindi
Jana, Zitto
alijibu kauli ya Lugola ya kumtaka aripoti polisi akibainisha kuwa atakwenda
ikiwa atapewa wito wa kisheria
Kupitia
ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter Zitto amesema, “waziri hana hayo
mamlaka. Kama polisi wananitaka watoe wito wa kisheria nitakwenda.”
“Naendelea na
kampeni za ubunge wa Buyungu ambapo tunamuunga mgombea wa Chadema na madiwani
wa ACT- Wazalendo kwenye kata kadhaa. Nashauri waziri ampate kwanza yule mbwa
wa polisi bandari.“
Rais John Magufuli ataja sababu za kumteua Kafulila
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment