Magufuli: Urais ni kazi ngumu


Rais John Magufuli amesema hakuna mwenye uhakika wa cheo katika serikali ya awamu ya tano hata yeye hana uhakika

Ameyasema hayo leo Agosti Mosi, wakati akihutubia mara baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa, makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu

Amesema kazi yake ni ngumu na wakati mwingine halali usiku au akaamshwa saa nane za usiku akipewa taarifa mbalimbali

“Hii ni kazi ngumu,   kama jana usiku nimeamka saa nane usiku IGP ananipigia simu anasema kuna watu wetu wamepata ajali mpakani, kuna mwingine anasema hivi. Basi na nyinyi mteseke kama mimi ninavyoteseka,” amesema

Amewaambia wateule hao hakuna anayeweza kukwepa kazi hiyo  na ana uhakika wana uwezo mkubwa wa kuwatumikia wananchi
Magufuli: Urais ni kazi ngumu Magufuli: Urais ni kazi ngumu Reviewed by KUSAGANEWS on August 01, 2018 Rating: 5

No comments: