Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), wamelaani kitendo cha kushikiliwa kwa
Wakili Mendrad D'Souza pamoja na wateja wake kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, Alexander Mnyeti na kudai hiyo ni sawa na kuzuia
mahakama isifanye kazi yake
Wakili huyo
maarufu wa kujitegemea jijini Arusha na wafanyakazi wanne wa kampuni ya
wakala wa pembejeo za kilimo Balton Ltd walikamatwa Julai 30 na kulazwa
mahabusu kwa saa 48 na waliachiwa jana jioni.
Akizungumza na
waandushi wa habari leo Agosti Mosi, Mratibu wa mitandao huo, Onesmo
Olengurumwa amesema THRDC wanatambua mawakili wanafanya kazi zao za utetezi kwa
mujibu wa sheria zilizowekwa na nchi
Hivyo
wanastahili kupewa ulinzi na uhuru wa kufanya kazi zao pasipo kuingiliwa na
mamlaka za serikali ili waweze kusaidia kutoa haki
"Mtandao
unaona kwamba madhara ya vitendo hivi yatakuwa makubwa na wananchi watashindwa
kupata haki yao ya kupata huduma na msaada wa kisheria kutoka kwa mawakili
iwapo vitendo hivi vitaendelea," amesema Olengurumwa
Kutokana na
hilo, ameshauri kwamba ikitokea kuna wakili viongozi anadhani amekiuka maadili
ya kazi yake basi atoe taarifa kwa chama cha mawakili au mahakama
Pia kwa
mawakili amewasihi kupitia vyama vyao wasimame kwa umoja na kulinda Uhuru
wa kazi ya mawakili na utawala wa sheria hapa nchini
Sambamba na
hilo, Mratibu huyo amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuacha kutumia
madaraka yao chini ya kifungu cha 15 na 17 cha sheria ya Tawala za Mkkoa ya
mwaka 1996 kwa kutoa amri ya kuwakamata watu na kuwaweka vizuizini bila sababu
za msingi za kisheria kwani vitendo hivyo vimekuwa vokijirudia mara kwa mara.
Mtandao walaani kukamatwa kwa Wakili Arusha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment