Rc Gambo awataka ma DC wapya kuacha Mihemko ya kiutendaji


Rc Gambo awataka ma DC wapya kuacha Mihemko ya kiutendaji
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewaasa wakuu wapya wa wilaya katika wilaya za Arumeru na Longido Kuacha Mihemko ya Kiuongozi kwa kutumia vibaya Madaraka yao kuwanyanyasa wananchi badala ya kuwaletea Maendeleo 

Aidha amewataka kutenda haki kwa wananchi ili kulinda heshima ya Rais Aliyewateua kwa kuzingatia ukomo wa madaraka yao na kuacha ujanja ujanja huku wakiwa na hofu ya Mungu.

Gambo ametoa rai hiyo mapema Leo Julai 31 wakati alipowaapisha wakuu hao wapya wa wilaya mbili za Mkoa wa Arusha ,ambapo alimwapisha Jerry Muro kuwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru na Frank Mwesumbe kuwa Mkuu wa wilaya ya Longido na kuwataka watumie ilani ya chama cha mapinduzi kutekeleza wajibu wao.

Aliwasihi kufanya maamuzi ya kiutendaji kwa kuzingatia ushauri wa wasaidizi wao wakiwa wanyenyekevu na kuacha kutumia ubabe kwa kuwaonea wananchi.

Akitolea mfano wilaya ya Arumeru yenye migogoro ya ardhi,alimtaka Mkuu huyo mpya kuitatua kwa kufuata sheria,taratibu,kanuni huku akizungatia weledi na uadilifu.

"Wilaya ya Arumeru ina Migogoro sana ya Ardhi lazima utatuzi wake unahitaji busara na ukienda Arumeru usiwe mkali wa kunyanyasa watu ila uwe mkali wa kutetea wananchi "
Amesema Gambo

Naye meya wa jijj la Arusha ,Kalisti Lazaro amewwataka wakuu hao wapya kutoa maelekezo,amri kwa kuzingatia sharia bila kukiuka taratibu.

Alisema kuwa wamepata madaraka wakiwa katika umri mdogo hivyo wanapaswa kutokuwangusha vijana wenzao ambapo hawakupata fursa hiyo ya kuwa viongozi kwa kutambua kuwa wao ni bora kuliko wngine

"Mnapotekeleza wajibu wenu mkumbuke kuwa mamlaka yenu yanaukomo na mnapowatumikia wananchi mzingatie sheria kanuni na taraibu huku mkimtanguliza mbele mwenyezi Mungu" Amesema Meya


Rc Gambo awataka ma DC wapya kuacha Mihemko ya kiutendaji Rc Gambo awataka ma DC wapya kuacha Mihemko ya kiutendaji Reviewed by KUSAGANEWS on July 31, 2018 Rating: 5

No comments: