Na
Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha
Alisema mbali na mafunzo kwa askari hao lakini
pia kwa kipindi cha wiki moja waliweza kutoa elimu kwa viongozi wa kata, vijiji
na vitongoji juu ya wajibu wao, wamiliki wa nyumba za kulala wageni, Bar na
Hoteli ambao wanatakiwa kuwa na leseni halali na kuhakikisha kwamba kumbi zao
zipo salama.
Aidha kwa upande wa madereva wa Bajaji na Boda boda walifundishwa mbinu za kupambana na uhalifu ikiwa ni pamoja na namna ya kutoa taarifa pamoja na sheria za usalama barabarani
Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha
Ikiwa ni siku 11 tu kupita toka
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng’anzi kuahidi kurudisha
utulivu katika tarafa ya Manyara wilayani Monduli, kwa sasa eneo hilo limezidi
kuimarika kiusalama baada ya kufanyika doria na operesheni za mara kwa mara na
jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu Mto wa Mbu
alizindua vikundi Tisa vya ulinzi shirikishi vilivyokuwa na jumla ya askari
215.
Awali Kamanda Ng’anzi aliitoa ahadi
hiyo alipokutana na viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji katika kikao
kilichofanyika ofisi ya Afisa tarafa tarehe 19 Julai mwaka huu ambapo viongozi
hao walisema suala linalosababisha kuwepo kwa matukio ya uhalifu ni uhusiano
hafifu baina ya baadhi ya askari Polisi, viongozi na wananchi hali ambayo
inatoa mwanya kwa wahalifu kuendelea kufanya uhalifu.
Baada ya kuwasikiliza kwa umakini
alibaini baadhi ya mambo ambayo yanayotakiwa yafanyike kwa haraka ikiwa ni
pamoja na kufanya doria na operesheni usiku na mchana, askari Polisi kutoa
huduma bora kwa wananchi hali ambayo itasaidia kuwa karibu nao na kupata
taarifa za uhalifu lakini pia uanzishaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi
katika kila kitongoji ambapo aliwahakikishia viongozi hao kwa kusema kwamba
eneo hilo litakuwa salama.
Kufuatia mikakati hiyo ya Kamanda
Nga’nzi ambaye alisema yeye anapenda sana kutenda badala ya maneno mengi, siku
hiyo hiyo aliongeza askari katika eneo hilo ambao walifanya operesheni katika
maeneo tete, kwenye bar na nyumba za kulala wageni lakini pia alipiga marufuku
kwa waendesha boda boda na Bajaji kufanya biashara hizo mpaka asubuhi.
Nao viongozi wa eneo hilo hawakuwa
nyuma na kuamua kumuunga mkono kwa kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi kama
jinsi alivyoagiza, ambavyo vilipewa mafunzo toka kwa Maofisa toka Kitengo
Polisi Jamii mkoa lakini pia kuahidi kutenga eneo na kujenga kituo kikubwa cha
Polisi.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na
umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo, aliwasitizia wananchi watoe ushirikiano wa
kutosha kwa askari hao kwa kuwafichua wahalifu ili taarifa zao zifanyiwe
kazi.
Kamanda Ng’anzi alikiri kuwepo kwa
upungufu wa askari Polisi na kusema kwamba uwepo wa vikundi hivyo vya Ulinzi
Shirikishi utasaidia kupunguza pengo hilo huku akisisitiza uwepo wa amani
utasaidia kukuza uchumi kwa wafanyabiashara wa eneo hilo ambao mara nyingi
wanawahudumia watalii wanaokwenda na kurudi toka katika vivutio mbalimbali.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo
cha Mafunzo cha JKT Makuyuni Luteni Kanali Phesto Mbanga aliahidi kushirikiana
na Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi eneo hilo la tarafa ya Manyara na
kuwasisitiza wananchi nao wasibaki nyuma kwani suala la amani ni wajibu wa watu
wote.
Awali akitoa taarifa juu ya mafunzo
hayo kabla ya kumkaribisha Kamanda wa Polisi, Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii
mkoa wa Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Edith Makweli alisema kwamba
askari hao walifundishwa namna ya ukamataji salama,upekuzi, haki zao wanapokuwa
kazini, silaha wanazotakiwa kutumia wakiwa kazini na Utii wa sheria bila
shuruti.
Aidha kwa upande wa madereva wa Bajaji na Boda boda walifundishwa mbinu za kupambana na uhalifu ikiwa ni pamoja na namna ya kutoa taarifa pamoja na sheria za usalama barabarani
AHADI YA RPC YAANZA KUTEKELEZWA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 31, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment