Rc Gambo awataka maDC wapya
kuacha Mihemko ya kiutendaji
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewaasa wakuu wapya wa wilaya
katika wilaya za Arumeru na Longido Kuacha Mihemko ya Kiuongozi kwa kutumia
vibaya Madaraka yao kuwanyanyasa wananchi badala ya kuwaletea Maendeleo
Aidha amewataka kutenda haki kwa wananchi ili kulinda heshima ya Rais
Aliyewateua kwa kuzingatia ukomo wa madaraka yao na kuacha ujanja ujanja huku
wakiwa na hofu ya Mungu.
Gambo ametoa rai hiyo mapema Leo Julai 31 wakati alipowaapisha wakuu
hao wapya wa wilaya mbili za Mkoa wa Arusha ,ambapo alimwapisha Jerry Muro kuwa
Mkuu wa wilaya ya Arumeru na Frank Mwesumbe kuwa Mkuu wa wilaya ya Longido na
kuwataka watumie ilani ya chama cha mapinduzi kutekeleza wajibu wao.
Aliwasihi kufanya maamuzi ya kiutendaji kwa kuzingatia ushauri wa
wasaidizi wao wakiwa wanyenyekevu na kuacha kutumia ubabe kwa kuwaonea
wananchi.
Akitolea mfano wilaya ya Arumeru yenye migogoro ya ardhi,alimtaka Mkuu
huyo mpya kuitatua kwa kufuata sheria,taratibu,kanuni huku akizungatia weledi
na uadilifu.
"Wilaya ya Arumeru ina Migogoro sana ya Ardhi lazima utatuzi wake
unahitaji busara na ukienda Arumeru usiwe mkali wa kunyanyasa watu ila uwe
mkali wa kutetea wananchi "
Amesema Gambo
Amesema Gambo
Naye meya wa jijj la Arusha ,Kalisti Lazaro amewwataka wakuu hao wapya
kutoa maelekezo,amri kwa kuzingatia sharia bila kukiuka taratibu.
Alisema kuwa wamepata madaraka wakiwa katika umri mdogo hivyo wanapaswa
kutokuwaangusha vijana wenzao ambapo hawakupata fursa hiyo ya kuwa viongozi kwa
kutambua kuwa wao ni bora kuliko wwngine
"Mnapotekeleza wajibu wenu mkumbuke kuwa mamlaka yenu yanaukomo na
mnapowatumikia wananchi mzingatie sheria kanuni na taraibu huku mkimtanguliza
mbele mwenyezi Mungu" Amesema Meya
Rc Gambo awataka Wakuu wapya Wa Wilaya Kutumia Vizuri Madaraka Yao
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 31, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment