"Kundi la Friends Of Batuli litakuwa Hazina ya Arusha na Tanzania ,Mengine yaige "Dkt Kihamia Mkurugenzi wa Nec
Aliyekuwa Mkurugenzi Wa Jiji LA Arusha ,Athumani Kihamia, ameeleza kuyatambua makundi Mbalimbali yanayofanya
kazi za kijamii katika jiji Arusha likiwemo kundi la Friends
Of Batuli kwa kuwa yamekuwa msaada Mkubwa kwa wananchi hasa kwa kuwa
kwamua na maisha Magumu.
Akizungumza na Kusaganews kwa njia simu katiika mahojiano maalum
Kihamia amesema analikubali kundi hilo la Friends of Batuli lenye Makao yake Makuu
Jijini Arusha amelisifu Kundi hilo kwa kuwa linakuja juu na linafanyakazi zake kwa mujibu Wa sheria na taratibu za nchini.
Amesema yeye ataendelea kutoa mchango wake kwa kundi Hilo kwa kuwa
limekuwa hazina kwa jiji la Arusha Pamoja na Nchi kwa ujumla
Awali Kihamia ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi
Wa Tume ya uchaguzi Nchini (NEC) ametajwa kuyapa
ushirikiano makundi hayo wakati alipokuwa Mkurugenzi wa Jiji
la Arusha jambo lililosaidia kupunguza changamoto za watu wenye kuhitaji msaada
wakiwemo watoto yatima
Moja ya Makundi hayo ni pamoja na Friends
of Batuli linaloongozwa na Mwl.Batuli Kisaya ambapo Kihamia
amedai kwamba kundi hilo linakuja vizuri tofauti na makundi mengine ambayo
yamekuwa mstari wa mbele kujinufaisha
Kihamia ameomba kundi hilo liungwe mkono kwa kuwa limekuwa la Mfano kwa uchapa
kazi Arusha
"Yapo Makundi Mengi ya kijamii katika jiji la Arusha
nayatambua ,ila hili kundi la Friends of
Batuli linakuja vizuri ni miongoni mwa makundi ambayo ni hazina ya
Arusha ninachoshauri lipanue mipaka zaidi na kufanyakazi na nje ya
Arusha katika kuhudumia jamii''Amesema Kihamia
Aidha Kihamia amewataka watumishi Wa halmashauri ya jiji la Arusha
wakiwemo wakuu Wa idara kutoa ushirikiano Wa dhati kwa
Makundi ya kijamii yenye mrengo wa kuwanufaisha wananchi yanapokuwa
yakitekeleza Majukumu yake
Ametoa wito kwa makundi mengine kuiga mfano Wa kundi la
Friends of Batuli na kuachana na dhana ya kuendesha
makundi kwa lengo la kujinufaisha .
"Kundi la Friends Of Batuli litakuwa Hazina ya Arusha na Tanzania ,Mengine yaige "Dkt Kihamia Mkurugenzi wa Nec
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment