Serikali imeahidi kutafuta fedha za dharura zaidi ya Sh2
bilioni za kukarabati kilomita saba za miundombinu ya maji katika mradi wa maji
wa Mugango-Butiama ili kuwawezeshia huduma wakazi wa Kijiji cha Kiabakari
wilayani Butiama kupata maji
Ahadi hiyo imetolewa leo Agosti 19 na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa alipozungumza na wakazi wa kijijini hicho
katika ziara yake mkoani Mara ya kutembelea na kukagua miradi iliyo chini ya
wizara yake
"Kuharibika kwa miundombinu hii kunasababisha upotevu
wa maji na kuwakosesha huduma wananchi; tutaitafutia ufumbuzi wa dharura kwa
kuufanyia ukarabati kusubiri mradi mkubwa wa maji utakaomaliza kabisa tatizo la
ukosefu wa maji katika wilaya za Musoma na Butiama," amesema Mbarawa
Miundombinu ya maji katika mradi huo unaotegemewa na wakazi
wa Kiabakari una urefu wa kilomita 19 ambaza saba zimeharibika na kusababisha
upotevu wa maji njiani
Awali, baadhi ya wakazi wa kijiji hicho walimweleza Waziri
Mbarawa kuwa tatizo la maji kijijini hapo linakwamisha maendeleo yao kiuchumi
kwa sababu wanalazimika kutumia muda mwingi kutafuta huduma hiyo badala ya
kushiriki shughuli za uzalishaji mali
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya Waziri na msafara
wake, Sabina Marwa na Isaac Jackson wameiomba Serikali kutekeleza kwa
vitendo kauli mbiu ya kumtwaa mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha kijiji hicho
kilicho umbali wa kilomita tisa pekee kutoka chanzo cha maji kinapata huduma ya
uhakika
"Wakati mwingine kijiji chetu kinapata huduma ya maji
ya bomba mara moja kwa mwezi licha kuwa kilomita tisa tu kutoka kwenye
chanzo," Jackson amemweleza Waziri
Serikali kutoa Sh2 billioni kutatua tatizo la maji Kiabakari
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment