Vyama vya CCM na Chadema vimewatangaza wagombea wao huku CCM wao
wakiwarudisha waliofukuzwa na Chadema ili kutetea tena kinyang’anyiro hicho
CCM wao imewarudisha waliokuwa madiwani wa kata hizo kwa
tiketi ya Chadema kabla ya kufukuzwa kwa kile kilichoelezwa ni utovu wa nidhamu
ambao ni Geofrey Kajigili (Sisimba), Newton Mwatujobe (Maanga), Mchungaji David
Ngogo (Nsalaga) na Hamphrey Ngalawa (Iwambia).
Akizungumza na gazeti hili leo katika ofisi za chama
hicho, katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Gerrald Mwadallu
amesema wagombea hao tayari wamekabidhiwa barua za
utambulisho zitakazopelekwa kwa watendaji wa kata na wanatarajia kuanza
kampeni za kuwanadi Agosti 24, 2018
"Tuna uhakika hawa wagombea wetu ni wachapa kazi na
wanatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya CCM chini ya Rais wetu John
Magufuli
“lakini kule walikokuwa walifanyiwa mizengwe kisa tu
wanaunga jitihada za viongozi wa CCM. Lakini sisi tunawarudisha hawa tukiamini
bado wanahitajika na wananchi wa kata husika, tunaomba waturudishie watu hawa
kwa maendeleo zaidi,” amesema Mwadalu
Kwa upande wa Chadema Mbeya Mjini, tayari kimewapitisha
wagombea wake kupitia kamati tendaji ya chama hicho baada ya kupigiwa kura za
maoni na wajumbe wa kata husika
Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu amewataja
wagombea wao na kata katika mabano ni Steven Mwashilindi (Maanga), Elisha
Mwandele (Iwambi), Odinary Sanga maarufu Pablo (Sisimba)
na Reward Mshanga
Mwaipalu amesema tayari wagombea hao juzi
walitambulishwa rasmi kwa wananchi wa kata husika na sasa wanachosubiri
ni kuanza kwa kampeni
“Kamati tendaji wilaya imezingatia matamanio ya wajumbe
waliopiga kura kwenye kata lakini imeonyesha wagombea walioshinda kwenye kura
za maoni wanapigiwa chapuo kubwa na wananchi wenyewe
“Hivyo na sisi tulipopitia sifa na uwezo wa kila mmoja
kulingana na kura walizopata, tuliridhika kwamba walioshinda kwenye kura za
maoni ndiyo wanaofaa zaidi kuwakilisha chama chetu kwenye kinyang’anyiro
hicho,” amesema
Uchaguzi huo wa Septemba 16, 2018 utahusisha majimbo
matatu ya Ukonga, Monduli na Korogwe Vijijini na na kata 21 nchini
Kumekucha uchaguzi mdogo Mbeya Mjini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment