Magari matano ya mizigo yameteketea kwa moto katika kituo
cha forodha Rusumo Wilaya ya Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda
baada ya gari la mafuta ya petrol kuligonga gari jingine na kupoteza
mfumo wa breki
Kwa mujibu wa shuhuda Chrispine Kamugisha amesema gari la
mafuta lilikuwa likiingia katika lango la forodha Rusumo na kupoteza mfumo huo
na baada ya kugonga lingine moto ulilipuka na kusababisha mengine kupatwa moto
huo na hakuna juhudi yoyote ya kuzima moto kwa kuwa ni mkali
Kamugisha amesema wananchi waliokuwa wakielekea makanosani
wamesambaza taarifa za ajali hiyo na limefika jeshi la polisi kituo cha Rusumo
na Kasulo kuondoa watu eneo la tukio huku madereva waliokuwa na magari eneo
hilo wameyasogeza mbali
"Eneo hili lina mteremko mkali kuingia sehemu ya
maegesho kufanya clearing kwenye ofisi za hapa hivyo hakuna kinachofanyika
kuzima moto huo hivyo serikali ichukue hatua kuweka zimamoto kwa wilaya
yetu," amesema Kamugisha
Matukio ya ajali ya magari katika kata ya Rusumo yamekuwa
yakitokea mara kwa mara baada ya magari kupoteza mfumo wa breki katika barabara
iendayo nchini Rwanda kutokana na miteremko mikali na kona nyingi ambapo
husababisha vifo majeruhi na kuteketea kwa mali mbalimbali
Kamanda wa polisi wilayani Ngara, Abeid Maige
amethibitisha kupokea taarifa za ajali hiyo na kwamba anaelekea huko
baada ya wenzake kutangulia walio jirani na eneo
Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael
amesema ukosefu wa zimamoto ni changamoto kubwa wilayani Ngara kutokana na
matukio ya ajali ya moto kuongezeka na ombi lilishatumwa serikalini lakini
utekelezaji wake haujafikiwa
Magari manne ya mafuta yawaka moto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment