KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhandisi Mussa Iyombe, ametaja sababu za wakuu wa
wilaya na wakurugenzi ambao uteuzi wao ulitenguliwa hivi karibuni.
Akizungumza jana katika kikao kazi cha wakuu wa wilaya
26 walioteuliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni, Iyombe alisema miongoni
mwa sababu za kutenguliwa huko ni kutojiheshimu
Alisema wakuu wa wilaya wengi waliondolewa ni kutokana
na kugombana na wabunge au wakurugenzi wa halmashauri
"Unamnyang'anya gari dereva unaendesha wewe au
wewe kazi yako ni kugombana tu na wabunge, wakati wewe una kazi zako na mbunge
ana kazi zake. Niwaambie tu ukweli wengi walioondoka ni kwa sababu hiyo.
Sasa wewe kila siku unagombana na mbunge, serikali gani hiyo ambayo inagombana
tu na wawakilishi wa wananchi,"alisema
Katibu mkuu huyo alisema wakuu hao wa wilaya
wanatakiwa kutengeneza mazingira ya haki ni haki na sheria ni sheria na si
kuwaweka ndani ovyo watu
"Umepewa mamlaka hayo lazima uyatumie vizuri
maana ukimweka ndani inapaswa kUnaweza kukuta labda tulikutana huko.
Tuligombana enzi hizo, sasa kwa kuwa umepata ukuu wa wilaya unasema ndio
atanikoma," alisema
Iyombe aliwataka kujiepusha na vitendo hivyo na
kutunza heshima ya Rais kwa kuwa ana imani sana na wao na anakasirishwa na hali
hiyo
"(Rais) ana vyombo vingi vya kukuangalia wewe.
Kwa hiyo mnatakiwa kuwa waanesho umfungulie mashtaka ya kijinai na ni lipi
sasa?
galifu kwenye hizi nafasi zenu. Niwaombe sana nyie
muwe ‘model’ (mfano).
Kama kuna mtumishi amekosea kuna mamlaka ya nidhamu,
iagize tu. Usiende pale ukamweka ndani kwani kuna sheria zinazomlinda huyo si
mwanasiasa," alisema
Alibainisha kuwa kama hajawajibika kuna mamlaka ya nidhamu
ya kushughulikia ni lazima kufuata sheria na taratibu zilizopo
"Serikali ina taratibu zake usiziruke na
kujiamulia. Angalia imekulinda kisheria, taratibu zimefuatwa hata kama wewe ni
mkono wa Rais," alisema na kuongeza kuwa mengi aliyoyaona kwa wakuu wa
wilaya waliokuwa wameteuliwa yalikuwa yanatia aibu
Wewe mkuu wa wilaya unaitisha kikao vizuri, unaenda
saa saba wakati kikao ni saa nne sasa unajenga heshima gani hapo? Unataka
uwafundishe nini uliowaita? Nimewatahadharisha haya mambo ya kiutendaji
tendaji," alisema huku akiwataka kutunza heshima ya Rais na wanatakiwa
kuwa mfano
Akifungua kikao hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tamisemi, Selemani, Jafo alisema akienda wilayani anakuta mkuu wa wilaya ki
vyake, mkurugenzi, mwenyekiti wa halmashauri, mbunge wilaya nzima inafanya kazi
kivyake
"Ukiacha wilaya ambazo nafasi zilizokuwa wazi,
hizi zingine zote ukifika uliza utaambiwa kulikuwa na hali gani na maeneo mengi
pale utakuta yule aliyeondoka aliyestaafishwa au kuondolewa kuna suala kubwa la
uhusiano,"alisema
Jafo alitaka wakajenge uhusiano na kufanya kazi na
kuwatii viongozi wao kwa kuwa maeneo mengine mkuu wa mkoa hataki mkuu wa wilaya
aonekane anafanya kazi na analijua hilo
Sababu ya Kutumbuliwa Ma DC na Wakurugenzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment