MAREKANI"Yatoa Kauli Kuhusu Uchaguzi Mdogo


Ubalozi wa Marekani umetoa tamko kuhusu uchaguzi mdogo wa jimbo moja na kata 77 uliofanyika Jumapili, ukieleza umepata taarifa za kuaminika kwamba ulighubikwa na vurugu na ukiukwaji wa sheria.

Taarifa iliyotolewa leo Agosti 15 kwa vyombo vya habari na Ofisi ya Habari ya Ubalozi huo, imeeleza kuwa ukiukwaji wa sheria katika uchaguzi huo ulihusisha kukataa kwa baadhi ya watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwasajili wagombea kutoka vyama vya upinzani

Pia taarifa hiyo imeeleza vitisho vya polisi dhidi ya wanachama wa vyama vya upinzani, watu kukamatwa kiholela bila kuwapo vibali vya ukamataji vilitawala katika uchaguzi huo wa marudio uliofanyika Agosti 12, 2018

Pamoja na hiyo pia imeelezwa kuwa kulikuwepo na ukandamizwaji wa uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni katika kipindi chote cha kuelekea uchaguzi huo. "Mambo haya yanakwaza haki ambazo Katiba ya Tanzania imewapa raia wake na kuhatarisha amani, utulivu na usalama nchini na eneo lote la kanda," imeeleza taarifa ya ubalozi huo

MAREKANI"Yatoa Kauli Kuhusu Uchaguzi Mdogo MAREKANI"Yatoa Kauli Kuhusu Uchaguzi Mdogo Reviewed by KUSAGANEWS on August 15, 2018 Rating: 5

No comments: