Upelelezi wa kesi inayomkabili mfanyabiashara anayetuhumiwa
kutaka kumpa rushwa ya Sh90 milioni Waziri William Lukuvi, bado haujakamilika
Mfanyabiashara huyo, ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya
Kiluwa Steal Group and Co. Ltd na Kiluwa Free Processing Zone anadaiwa kutaka
kumpa rushwa hiyo Lukuvi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi
Hayo yameelezwa leo Agosti 15 na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Huduma Shahidi wakati kesi hiyo ilipotajwa
Wakili Ndimbo amedai mahakamani hapo kuwa upelelezi bado
haujakamilika na kwamba kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na akaomba ipangiwe
tarehe nyingine ili kuangalia kama ushahidi utakuwa umekamilika au la
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shahidi
aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 14, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa
Mshtakiwa huyo ambaye yupo nje kwa dhamana
Katika kesi hiyo mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Julai 16,
mwaka huu kati ya saa 6 na saa 8 mchana akiwa mkurugenzi wa kampuni hizo mbili
alitoa rushwa ya Dola 40,000 za Marekani ( Sh90 milioni) kwa Waziri Lukuvi
Kesi ya aliyempa Waziri Lukuvi rushwa yagonga mwamba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment