Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na
viongozi wa dini za kikristo nchini
Katika mazungumzo yao Rais amewataka kufanya kazi na
kuendelea kuhubiri kuhusu amani, upendo na mshikamano
“Nawahakikishia mimi nipo pamoja na nyinyi, nendeni mkafanye
kazi kwa kujiamini na kwa uhuru, mkiwa na jambo lolote nijulisheni
nitalishughulikia, wahubirieni Watanzania amani, upendo, mshikamano na kuipenda
nchi yao,” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Agosti, 7 2018 alipokutana
na viongozi wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania na
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) waliokwenda Ikulu jijini Dar es
Salaam kujitambulisha kwake
Viongozi hao ni pamoja na Mwenyekiti wa CCT Askofu Anilikisa
Cheyo, Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa CCT Askofu Fredrick Shoo, Makamu
wa Pili wa Mwenyekiti CCT Askofu Jacob Chimeledya na Katibu Mkuu wa CCT
Mchungaji Moses Matonya
Wengine ni Rais wa TEC Askofu Gervas Nyaisonga NA
Makamu wa Rais TEC Askofu Flavian Kasalla
Taarifa kutoka KWA Mkurugenzi wa Mawasiliano IkulU, Gerson
Msigwa imesema kuwa Rais amekutana na kujadilina na viongozi hao
kuhusu ushirikiano
Rais Magufuli amewashukuru kwa dhamira yao ya kutaka
kukutana nae na kufanya naye mazungumzo na amewahakikishia kuwa Serikali
inatambua mchango mkubwa wa madhehebu ya dini na taasisi zake
Amesema serikali itaendelea kushirikiana nayo katika
kuwahudumia na kuwaletea maendeleo wananchi
Anaeleza katika mazungumzo hayo viongozi hao wamemhakikishia
utayari wao wa kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali, kuyasimamia
makanisa yao ili yaendelee kutoa huduma ya kiroho na kijamii kwa manufaa ya
Watanzania wote na kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazojitokeza
Pia viongozi hao wamempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa
zinazofanywa na Serikali ya wamu ya tano katika kuleta maendeleo na kuimarisha
huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya usafiri na majengo, kuleta
nidhamu katika utumishi wa umma, mapambano dhidi ya rushwa
“Wamempongeza pia kwa kuimarisha usimamizi wa rasilimali za
Taifa hasa madini, kupambana na wizi na ufisadi wa mali za umma, kutoa elimu ya
msingi na sekondari bila malipo, kuimarisha huduma za afya
na kuwapigania wakulima,” imesema taarifa hiyo
Viongozi hao wamewaomba watanzania wote kumpa ushirikiano wa
kila aina Rais Magufuli kwa kuwa wanatambua na wameona kazi nzuri
anayoifanya
Rais Magufuli akutana viongozi wa dini Ikulu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment