Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), kupitia Jumuiya ya Wazazi (UWT) Namelok Sokoine
ameibuka na kudai kwamba yeye si mwanasiasa msaka tonge kama ilivyo kwa wasiasa
wengine.
Kauli hiyo ameitoa mjini hapa baada
ya kudaiwa kuhusika katika mpango wa kuandaa baadhi ya wana CCM waliovamia
ofisi za chama hicho Wilaya ya Monduli wakipinga mpango wa kupendekeza jina la
mwanachama mpya wa CCM, Julius Kalanga, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia
Chadema.
Akizungumza na Mtanzania Digital,
Sokoine aliyegombea ubunge kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 akichuana na
Kalanga amesema, kwa kawaida yeye ni mwanasiasa na mtu asiyejificha hivyo kama
angekuwa na nia ya kutaka kugombea kwenye uchaguzi mdogo hilo lisingekuwa
tatizo kwake.
“Watu wasiogope vivuli vyao, mimi si
mtu wa kujificha mwaka 2015 nilisimama kukipigania chama changu ingawa wengine
walikimbia kusaka tonge, hivyo utaona kwa jinsi gani mimi si msaka tonge ni
mwana CCM ninayekipenda na kukitahimini chama changu.
“Hao wanaodai kwamba wananchi
waliofika Ofisi za CCM wilaya kuelezea kero zao kuhusu kanuni kuwa wanatoka
kata za marafiki zangu naomba niwaambie hizo si kata za mtu ni kata
zinazoongozwa na CCM na ndiyo zilizompa ushindi Rais John Magufuli mwaka 2015,”
amesema.
NAMELOK: MIMI SI MSAKA TONGE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment