Mkuu wa wilaya
ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wataalamu wa afya wilayani humo kutoa
elimu ya njia sahihi za kunyonyesha watoto
Amesema elimu
hiyo itawawezesha kinamama kupata kizazi chenye afya bora na kushiriki vyema
masuala ya uchumi na kijamii kwa siku zijazo
Ameyasema hayo
leo Agosti 7 muda mfupi mara baada ya kufunga maadhimisho ya wiki ya
unyonyeshaji watoto duniani yaliyofanyika mjini humo kwa ngazi ya wilaya ya
Kisarawe
Hii ni kazi ya
kwanza kwa Jokate tangu ateuliwe na kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe
"Uongozi
wa Serikali kwa ngazi zote mnapaswa kuweka misingi imara na kuhamasisha jamii
yetu ili itilie maanani kunyonyesha watoto kikamilifu."
Jokate
amewakumbusha waajiri kuzingatia sheria za ajira zinazowataka kuwapa likizo ya
uzazi ya siku 84 ili waweze kunyonyesha watoto wao kikamilifu
"Hii si
kwa upande wa kinamama pekee bali hata kinababa nao wanapaswa kupewa likizo ya
uzazi ya siku tatu pindi wake zao wanapojifungua na hizo siku wanapaswa
wazitumie kuwapa misaada mbalimbali wake zao ili waweze kunyonyesha watoto wao
kikamilifu," alisema Jokate
Awali mratibu
wa lishe wilayani humo, Mwanaharusi Issa alisema takwimu zinaonyesha kuwa
watoto wenye umri wa miaka mitano wenye utapiamlo mkali katika wilaya ya
Kisarawe ni asilimia 0.7 huku wenye utapiamlo wa kadri ni asilimia 13.6.
Mwanaharusi
amesema ili kupunguza tatizo la utapiamlo lililopo, wataalamu wa afya
wanatakiwa kumuelekeza mama jinsi ya kumpakata mtoto na kumweka kwenye titi
ipasavyo mara baada ya kujifungua
Pia
kumuelekeza mama aliyejifungua jinsi ya kukamua maziwa yake ili mtoto aweze
kupatiwa pindi anapokua mbali
Naye meneja wa
mradi wa chakula na lishe kutoka shirika lisilo la kiserikali la Feed the
Children, Silvia Imalike amesema takwimu za utafiti wa hali ya
kidemografia na afya uliofanyika mwaka 2015 zinaonyesha kuwa asilimia 59 ya
watoto wa umri wa miezi 0 hadi miezi 6 nchini wananyonyeshwa maziwa ya mama
pekee
Hii ndiyo kazi ya kwanza ya Jokate
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment