Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu
ameruhusiwa kutoka hospitalini alipolazwa kuanzia leo ataishi nyumbani
Tangu Septemba 7 mwaka jana aliposhambuliwa kwa risasi zaidi
ya 30 jijini Dodoma, Lissu amekuwa akiishi hospitalini kwa matibabu zaidi
Ujumbe wa Lissu alioutoa leo Agosti 7, 2018 ameanza kwa
kusema; “Hello Friends of Me!!! Good afternoon to y'all. Kwa mara nyingine
nawaleteeni habari njema."
Amesema alfajiri ya Januari 6, 2018 aliondoka Hospitali ya
Nairobi nchini Kenya na kusafiri hadi Leuven nchini Ubelgiji, kwa ajili
ya matibabu zaidi
Lissu amesema jana Agosti 6, 2018 alitimiza miezi saba tangu
alipowasili nchini humo
“Leo Agosti 7 ni miezi 11 toka siku niliposhambuliwa na watu
wanaojulikana sana kama 'watu wasiojulikana.'"
"Septemba 7 mwaka jana sikulala nyumbani kwangu. Agosti
7 ya leo, miezi 11 kamili baadae, nimeamkia nyumbani kwangu," amesema
Lissu
Ameongeza: "Septemba 7 iliyopita wote mlikuwa na
hofu kubwa kama ningemaliza siku hiyo au siku chache zilizofuata, nikiwa hai.
Miezi 11 kamili baadae, Professor Dk Wilhelmus Jan Mertsemakers, daktari wangu
tangu nilipokuja University Hospital Leuven, amesema sina sababu ya kitabibu ya
kuendelea kukaa hospitali."
"Profesa Mertsemakers amesema nitaendelea na uponyaji
nikiwa nyumbani kwangu. Nitatembelewa na wauguzi kila siku nyumbani
kuniangalia naendeleaje. Na nitarudi hospitali kumwona kila baada ya wiki
mbili," amesema Lissu.
Katika ujumbe huo, Lissu ameendelea kusema, bado ana
chuma kubwa kwenye paja .
“Liko kama antenna ya
TV za mwaka '47 na Profesa Mertsemakers amesema nitakaa nalo kwa si chini ya
miezi sita. Lakini habari ya mujini ndio hiyo: nimetoka
hospitalini."amesema
Amemaliza kwa kusema: "Hongereni sana kwa kazi
nzuri ya kuniuguza na kuniponya na chochote mtakachokula au kunywa siku ya leo
mnibakishie. Siko mbali
Lissu aruhusiwa kutoka hospitalini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment