Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amewataka wote
wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya Ruvu Kusini na
Kazimzumbwi wilayani humo kuondoka mara moja kabla hajatumia nguvu
Jokate ametoa agizo hilo leo Agosti 7 akiwa kwenye msitu wa
Ruvu Kusini ambako alienda na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa
wa Wakala wa Misitu ( TFS) kwa ajili ya kuwaondoa wavamizi waliopo humo
Akiwa ndani ya msitu wa Ruvu Kusini Jokate amezindua
operesheni ya kuwaondoa wavamizi na kuipa jila la "Operesheni
Jokate".
Amesema lengo lake ni kuwasaka na kuwaondoa wavamizi ambao
hawataki kufuata sheria na utaratibu wa hifadhi ya misitu katika msitu wa Ruvu
Kusini uliopo wilayani humo
Jokate amesema operesheni hiyo ni ya siku sita na imeanza
leo Agosti 7 ambapo katika siku ya kwanza ng'ombe zaidi ya 150 walikamatwa
ndani ya msitu huo na zoezi la kuwakamata wamiliki wake linaendelea
"Kwa kuanza na utekelezaji wa maagizo ya mkuu wa mkoa wa
Pwani, Evarist Ndikilo nimeamua nianze msitu huu wa Ruvu Kusini baada ya kupata
dondoo ya kuwepo wavamizi,” amesema
Amesema atahakikisha anasimamia na kuona kazi hii inakwenda
vizuri na misitu yote inaendelea kulindwa na kuwa katika hali nzuri
Amewataka wakazi wanaoishi maeneo ya jirani na msitu huo
kuheshimu mipaka na taratibu zilizopo ili kuepuka kuingia kwenye mkono wa
sheria
Kwa upande wake, Meneja wa TFS Kanda ya Mashariki, Caroline
Makundo amesema msitu huo umevamiwa kwa shughuli za kilimo na ufugaji kwa
maaana ya mifugo kuingizwa humo na kwamba kazi ya kuwasaka wavamizi itafanyika
usiku na mchana kwa siku hizo sita
Jokate aanza Oparesheni Rasmi na Kumtambulisha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment