Polisi Watinga Kijijini cha Ngole Kukamata Wananchi Baada ya Agizo la Rc


Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, kuliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwaweka ndani wananchi wote wa Kijiji cha Ngole, utekelezaji wa agizo hilo umeanza na tayari polisi wametinga kijijini huko

Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Mateo, amesema magari kadhaa yametumwa yakiwa na askari wa kutosha kwa ajili ya kuwakamata wananchi hao

Amesema kitendo kilichofanywa na wananchi wa kijiji hicho ni uhujumu uchumi, hivyo ni lazima washughulikiwe ipasavyo.

Amesema baada ya agizo la Mkuu wa Mkoa, jeshi hilo lilipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika

Polisi Watinga Kijijini cha Ngole Kukamata Wananchi Baada ya Agizo la Rc Polisi Watinga Kijijini cha Ngole Kukamata Wananchi Baada ya Agizo la Rc Reviewed by KUSAGANEWS on August 16, 2018 Rating: 5

No comments: