Mtuhumiwa afikishwa mahakamani Akiwa na majeraha yake


ALIYEKUWA msaidizi wa mgombea udiwani wa Kata ya Kaloleni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ibrahim Issa (32), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha akiwa na majeraha yake, kwa tuhuma za kumjeruhi Idd Musa

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali, Mary Lucas alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Chrisanta Chitanda, alidai mtuhumiwa huyo alimjeruhi Iddi Mussa Agosti 12, mwaka huu, katika eneo la Kaloleni

Alidai kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alimjeruhi kwa kumchoma kisu mkono wa kushoto Musa na kumsababishia jeraha.

Wakili huyo aliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyingine kutokana na upelelezi wake kutokukamilika

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo

Mtuhumiwa anayetetewa hapo na Wakili SheckMfinanga, aliachiwa baada ya kudhaminiwa na watu wawili ambao kila mmoja alitia saini hati ya dhamana ya thamani ya Sh. milioni mbili

Hakimu Chitanda aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 17 mwaka huu itakapitajwa tena

Agosti 12 majira ya saa nne asubuhi katika Kata ya Kaloleni, vyombo vya habari viliripoti msaidizi wa mgombea udiwani, Ibrahimu Issa, alijeruhiwa kwa kuchomwa kisu jicho la kushoto na sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekwa katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, ambako aliondolewa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi hadi jana alipofikishwa mahakamani

Mtuhumiwa afikishwa mahakamani Akiwa na majeraha yake Mtuhumiwa afikishwa mahakamani Akiwa na majeraha yake Reviewed by KUSAGANEWS on August 16, 2018 Rating: 5

No comments: