Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro
Mambosasa amesema polisi imeanza uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa mwandishi wa
habari wa Wapo Redio, Sillas Mbise
Mbise anadaiwa kushambuliwa na polisi juzi Agosti 8, 2018
wakati wa mchezo kati ya Simba na Asante Kotoko ya Ghana
Video za tukio hilo zimesambaa katika mitandao ya kijamii,
zikimuonyesha Mbise akishushiwa kipigo na polisi
Akizungumza leo Ijumaa Agosti 10, 2018 Mambosasa amesema
polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kufungua jalada la uchunguzi wa
picha hizo za video
Amesema hiyo inakwenda sambamba na kumtaka mtendewa wa kosa
hilo la kupigwa kutoa taarifa kituo cha polisi ili hatua stahiki ziweze
kuchukuliwa
Amesema mtu yeyote anatakiwa kutoa malalamiko yake pale
anapoona ametendewa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria
Polisi wachunguza kupigwa mwanahabari
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment