Halmashauri Monduli Rasmi Kurejea CCM kutokana na Hili.


Unaweza kusema halmashauri ya Monduli Mkoa wa Arusha ambayo ilikuwa inaongozwa na Chadema imerejea CCM baada ya madiwani 10 wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini kujiuzulu na kujiunga na chama tawala

Akizungumza leo Jumamosi Agosti 11, 2018 mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Steven Ulaya amesema baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Chadema walipata madiwani 18, wakiwemo wa viti maalum watano huku CCM ikipata madiwani tisa, wawili wakiwa wa viti maalum

“Tayari CCM imeshinda kata sita katika chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika, bado kuna uchaguzi katika kata mbili, ikiwemo ya Monduli baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo kujiuzulu. Pia aliyekuwa mbunge (wa Chadema Monduli-Julius Kalanga) amejiuzulu,” amesema

Amesema kwa sasa Chadema imebaki na madiwani tisa, wakiwemo watano wa viti maalum

Akizungumza wimbi la madiwani kujiuzulu, Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Aman Golungwa amesema kinachofanywa na wanaohama ni mchezo mchafu, kusisitiza kuwa chama hicho hakiwezi kufa, “waache waondoke ila wananchi wanajua kinachoendelea.”

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema wanaotaka kuondoka katika chama hicho wasijifiche, kuwataka watoe taarifa na wataagwa

“Tunasema waache waondoke kwa ajili ya shida zao binafsi sisi tutabaki na kamwe wasidhani Chadema itakufa,” amesema
Mpaka sasa madiwani 31 wa Chadema mkoa wa Arusha wamejiuzulu na kujiunga na CCM.
Halmashauri Monduli Rasmi Kurejea CCM kutokana na Hili. Halmashauri Monduli Rasmi Kurejea CCM kutokana na Hili. Reviewed by KUSAGANEWS on August 11, 2018 Rating: 5

No comments: