Kamati tendaji ya Chadema Wilaya ya Mbarali(Mbeya)
imemfuta uanachama na kumvua udiwani, Diwani wa Kata ya Ruiwa, Kassim
Mtale kwa madai utovu wa nidhamu, usaliti na kukiuka taratibu na kanuni za
chama hicho
Akizungumza Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbarali, Nicolaus
Lyaumi amesema katika kikao chao walichoketi Alhamisi wiki hii walijiridhisha
kwamba Mtale amekiuka taratibu za chama hicho, hivyo wakakubaliana kumfuata
uanachama na kumvua udiwani
"Kweli tulishamfuta uanachama na kumvua udiwani, kuna
mambo mengi yalifanyika dhidi yake ya usaliti, utovu wa nidhamu, sasa Chadema
ni taasisi ya umma sio mtu mmoja. Kutokana na hayo chama kimeamua kumfuta
kabisa uanachama," amesema Lyaumi
Hata hivyo, Mtale mwenyewe kasema hajafukuzwa ila amejivua
uanachama na udiwani kwa hiyari yake na kujiunga na CCM.
Amesema ameamua kwenda CCM akiamini kwamba huko ataweza
kuwatumikia vyema wanannchi wake tofauti na akiwa Chadema au chama chochote cha
upinzani
Amesema; ‘Sisi vijana tuliingia huku (Chadema) tukiwa na
matumaini makubwa kwamba kutakuwa na fursa nyingi, lakini nimeona yale yote
tuliyokuwa tunayahubiri ndiyo yanayotekelezwa na Rais wetu John Magufuli. Hivyo
na mimi sina budi kumfuata ili kuongeza nguvu zaidi”
Chadema wamfuta uanachama diwani wake Mbeya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment