Wanasiasa na
baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini wametoa maoni tofauti kuhusu
uamuzi wa mwanasiasa Julius Mtatiro aliyetangaza kuhama CUF na kuonyesha nia ya
kuhamia CCM
Mtatiro ambaye
alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, amewaambia wanahabari leo
Agosti 11, 2018 jijini Dar es Salaam kwamba, amejiuzulu CUF na yuko tayari
kujiunga na CCM kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Magufuli
Saa chache
baada ya kutangaza uamuzi huo, wanasiasa mbalimbali waliibuka na kuandika
kwenye mitandao ya kijamii wengine wakimpongeza na wengine wakimkosoa
Mbunge wa
Kigoma Mjini, (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe ameandika kwenye ukurasa wake wa
Twita ameandika akisema
“Huko
wanakokutegea kukufukuza kila usemapo ukweli? Ninaamini kwenye maendeleo ndani
ya Demokrasia na siyo maendeleo ndani ya udikteta. Ninaamini katika uhuru wa
fikra na siyo mawazo ya kiimla.Ninaamini nchi yetu inahitaaji chama kingine kuirudisha
kwenye reli. Nafasi ya CCM ni Museum (makumbusho
Mbunge wa
Nzega, (CCM) Hussein Bashe ameujibu ujumbe wa Zitto akisema
“Ni
rahisi kuleta mabadiliko ya haki, demokrasia na maendeleo ndani ya CCM) kuliko
kutafuta mabadiliko nje kwa sababu kuna mgogoro wa kimawazo, kimuundo na
kimadili huko nje. Kuna wanajeshi wachache wa ukweli.”
Kwa upande
wake, Nape Nnauye Mbunge wa Mtama (CCM) ameandika akisema
“Tunachagua
rangi ya Paka wakati shida yetu ni kukamata Panya.Nguvu tunayopoteza kuhoji
rangi ya paka ingetumika kushughulika na panya tungekuwa mbali sana,”
Nape katika
nukuu yake nyingine ameandika akisema
“Kama msomi wa
Sayansi ya Siasa, naona hii ni fursa muhimu ya kujengwa kwa aina mpya ya vyama
na siasa za upinzani nchini. Kwa demokrasia, hamahama hii muhimu itumike kama
fursa ya kujenga upya uimara wa CCM unaotegemea ubora wa upinzani(Simba/Yanga).
Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole yeye ameandika
“Huu unaitwa
uhuru wa kisiasa kwa mujibu wa katiba yetu, halafu wale wa ‘siasa za bei nafuu
mseme kanunuliwa;” Hongera kaka, ndugu, kamaradi. Historia na Mungu pekee
atakupa tuzo ya dhamira yako njema. Na mimi nimeikuta mtandaoni.”
Bashe, Nape, Zitto, Polepole wajadili kuondoka Mtatiro CUF
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment