Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro
Mambosasa amesema polisi waliokuwa zamu siku ambayo mwandishi wa habari wa Wapo
Redio, Sillas Mbise alishambuliwa na askari, wameanza kuchunguzwa
Mbise anadaiwa kushambuliwa na polisi juzi Agosti 8, 2018
wakati wa mchezo kati ya Simba na Asante Kotoko ya Ghana uliofanyika katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Amesema jukumu la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali
zao na si kuwapiga raia waliotenda kosa ambao hawajakataa kutii sheria ya
kukamatwa
Mambosasa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Agosti 10, 2018
katika mkutano na waandishi wa habari, ikiwa ni baada ya kusambaa kwa video za
tukio la kupigwa kwa mwandishi huyo katika mitandao ya kijamii, zikimuonyesha
akishushiwa kipigo na polisi wawili
“Tayari jeshi la polisi limefungua jalada la uchunguzi
kuhusiana na tukio hili ili kubaini ukweli na tayari askari waliokuwa zamu eneo
la tukio wameanza kuchunguzwa ikiwamo wawili kuhojiwa,”amesema Mambosasa
Amesema pamoja na uchunguzi kuanza polisi wanamtaka
mwandishi huyo kutoa taarifa kituo cha polisi ili hatua stahiki ziweze
kuchukuliwa
“Tunamtaka mwandishi huyo kutoa taarifa kituo cha polisi ili
hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa kuwa mtu yeyote anatakiwa kutoa malalamiko
pale anapoona anatendewa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria,”amesema
Mambosasa
Askari wawili wahojiwa tukio la mwanahabari kupigwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment