Leo ninawaletea ufafanunuzi wa mambo yanayoashiria
ufanano wa kiutendaji kati ya Mwl Nyerere na Ndg Magufuli Mwkt wa CCM na Rais
wa Tanzania, kwa kuwa viongozi hufananishwa na hutofautishwa kwa utendaji wao
katika kutoa uongozi.
-Ukweli
Mwalimu mwanzoni mwa miaka ya 1960 alipojiuzulu Uwaziri
Mkuu kwenda kujenga Chama nakumuachia Serikali Mzee Kawawa, aliandika vitabu
vitatu kimojawapo ni TUJIJISAHIHISHE ni kitabu kidogo chenye kurasa
zisizozidi ishirini ambapo amesisitiza
katika kusema kweli na neno Kweli limetajwa zaidi ya mara ishirini.
"Ukweli unatabia moja nzuri sana, haujali mkubwa
wala mdogo, haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo
tabia ya kujilipiza kisasi kama
ukipuuzwa.."
Hayo ni baadhi ya maneno katika kitabu hicho,
yanayosisitiza kusema ukweli na kuheshimu ukweli. Hii ni sawa kabisa kwa
Magufuli ambaye toka awali amekuwa ni kiongozi anayesisitiza kusema ukweli na
kwa sasa ni mwasisi wa msemo "Msema kweli ni mpenzi wa Mungu".
-Kusimamia Misingi
CCM ina msingi wa vitu viwili, Haki na Watu. Mwalimu
mwaka 1968, akitoa hotuba aliyoiita, "Lazima Chama Kiwasemee watu" na
moja ya kauli zake ni, "kazi ya Chama cha Siasa kilicho imara ni lazima
kiwe kama daraja la kuwaunganiaha watu na serikali walioichagua." Mwalimu
alisema akiwaasa viongozi wa Chama kuwa karibu na wananchi na kuwa watetezi wa haki za wanyonge.
Hiyo tunaishuhudia tena kwa Magufuli ambapo kwa kiasi
kikubwa amekuwa akiwasisitiza viongozi
wa Chama kuwa sikio la wananchi na hata mageuzi ya Chama yamelenga kukifanya
kuwa "Chama Cha wanachama na kinachoshughulika na shida za watu"
-Falsafa ya kazi
Mwaka 1976 Mwalimu aliandika kitabu "kila mtu
afanye kazi" kinachoeleza kwa undani umuhimu wa kazi katika maisha binafsi
na kwa taifa. Sasa ni miaka 40 Magufuli amekuja na falsafa inayofanana ya
"Hapa Kazi Tu".
- Sera ya Viwanda na Kilimo
Mwalimu aliweza kuanzisha programu za kilimo ikiwemo
"utekelezaji wa siasa ni kilimo" - 1974, sera ya viwanda vidogo
vidogo (SIDO), vya kati ikiwemo viwanda vya nguo urafiki, Mwatex, Mutex,
Mbeyatex, n.k Sawa kabisa na Magufuli ambaye ndoto yake ni Viwanda. Miezi
miwili iliyopita amezindua mradi mkubwa wa kilimo awamu II utakaogusa maisha ya
wakulima wadogo kwa kuwapatia mikopo nafuu ya kilimo.
-Udhibiti wa madini
Katika suala la madini Mwalimu alifanya utambuzi wa
maeneo yenye madini, hakuruhusu uchimbaji uanze mbali na changamoto tulizokuwa
tukizipitia kama Taifa, kwa kuwa Watanzania hatukuwa na elimu ya kutosha ya
Madini. Magufuli amekuja amekuta mikataba kandamizi iliyoingiwa na watangulizi
wake baada ya mwalimu hivyo ameifumua mikataba yote ya Madini na kufanya haki
ya mtanzania kuheshimiwa na kuweza kuingia makubaliano kutoka 3% ya awali mpaka
50/50%.
- Reli, Umeme na Anga.
Mwalimu aliweza kujenga Reli ya TAZARA miaka ya 1970,
kwa upande mwingine alikuwa na ndoto kubwa ya ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme
maarufu kama Stiegler's Gorge ambao ulikwamishwa, shirika la ndege lilikuwa na
ndege za AirTanzania kabla halijafa katika awamu zilizofuata. Miaka 30 sasa
Magufuli amefufua shirika la ndege na mpaka sasa serikali imefanikiwa kununua
ndege Saba ndogo za kati na kubwa. Ujenzi wa Reli ya kisasa unaendelea naujenzi
wa mradi mkubwa wa umeme wa Stiegler's Gorge umeanza.
Vijana wa miaka ya 1990, Nyerere tunayesimuliwa
nakumsoma amerejea katika sura ya Magufuli na ni jukumu letu kumpa ushirikiano
na kufanya naye kazi kuhakikisha tunatekeleza na kufikia ndoto ya TViwanda.
Na mwandishi wetu,
Said Said Nguya
Saidnguya@gmail.com
NYERERE ANAISHI KATIKA SURA YA MAGUFULI.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment