Waziri wa
Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala leo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa
akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anakotibiwa
Dk Kigwangala,
leo Agosti 7, anatimiza miaka 43 ya kuzaliwa kwake
Waziri huyo
alipata ajali ya gari Agosti 4 mwaka huu eneo la Magugu, Manyara
Ameandika
katika ukurasa wake wa twitter akimshukuru Mungu kwa kufikisha umri huyo
“Leo
ninatimiza miaka 43 toka nizaliwe. Ahimidiwe Allah aliye Mkuu kuwa bado nipo
hai mpaka sasa. Najua ni kwa utashi na kusudio lake. Namshukuru na nazidi
kuomba kwake shufaa, siha na mafanikio tele. Ninawashukuruni nyote kwa dua
zenu. Tudumu kwenye sala ndugu zangu.” Ameandika
Pia, ameutumia
mtandao huo, kumkumbuka Ofisa Habari wa Wizara yake, Hamza Temba aliyefariki
dunia katika ajali hiyo
“Nimeangalia
simu yangu na kukutana na picha za ziara yetu ya PoriKwaPori na ndiyo nauona
ukweli kuwa mdogo wangu, bwashee wangu, huyu kijana mdogo mchapa kazi na
aliyekuwa na matumaini makubwa, sitamuona tena na kumtania,” ameandika
Akaongeza:
“Niseme nini tena? Qaalu inna lillah wainna ilayhir rajiuun,”
Kigwangala asherehea siku ya kuzaliwa Hospitali, amlilia Hamza Temba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment