Kalanga Apingwa na Wananchi wa Monduli

MAMIA ya wakazi kutoka kata mbalimbali wilayani Monduli, wamefika ofisi za CCM za wilaya hiyo wakimtuhumu Mwenyekiti wa CCM Wilaya kufanya njama za kumtaka aliyekuwa mbunge wa chadema Julius Kalanga kuwa mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi

Mkazi wa Kijiji cha Esilaley, Sairey Loboye, alisema mwanachama ye yote mpya akitaka kugombea nafasi za uongozi, anatakiwa kuandika barua ya maombi ambayo itajadiliwa na vikao vya chama sasa ajabu in kwamba viongozi wa ccm wamempitisha kinyemela na sisi hatumtaki

Hata hivyo, alisema kanuni za chama zinataka mwanachama mpya kukaa mudas wa miaka mitatu chini ya uangalizi wa chama kabla ya kupitishwa kuwa mgombea wa nafasi ya uongozi.

“Sasa hawa wanaojiunga leo na kupitishwa kuwa wagombea leo leo tutajuaje kama siyo mamluki wa kuvuruga chama,” alisema.

Alisema kuna madai tayari baadhi ya viongozi wa mila (malaigwanani), wameanza kumpigia debe mwanachama mpya apitishwe kuwa mgombea ubunge.
“Hii ni kutuvuruga,” alisema.
Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Sepeko, Nooy Naimisye, alisema jana kuwa wanataka kuona demokrasia ikitendeka katika kumchagua mgombea ubunge katika jimbo hilo.
“Mwenyekiti atupe ukweli kuhusu madai kwamba yupo upande wa mbunge wa zamani aliyejiuzulu Chadema na kutangaza kujiunga CCM.
“Tunataka demokrasia, hatuna nia kuona mgombea huo anagombea tena kwenye chama chetu, hii ni kinyume na kanuni na utaratibu ndani ya chama,” alisema.
Alisema upo utaratibu wa mwanachama kujiunga na CCM na kisha kupewa ridhaa ya kugombea, anayejiunga sasa hivi asichukuliwa kuwa ni wa maana sana.
“Upo utaratibu mzuri tu wa chama, mtu wa aina hiyo anatakiwa kukaa miezi mitatu
Kwa upande wake, mwanachama kutoka Kata ya Monduli Juu, Daniel Leyani, alisema, wanachama wapewa haki yao ya kumchagua mgombea ambaye wanamtaka na siyo kupewa mgombea kwa shinikizo la viongozi.

Mkazi wa Kata ya Moita, Lekinye Lisasi, alisema tatizo lipo katika mitaa, ambako imesikika kuwa wapo viongozi wa CCM wilaya ambao wameshaonyesha kumtaka mwanachama mpya kugombea.
Mwenyekiti wa tawi la Tenki la Maji, lililopo Kata ya Silale, Hamis Abdallah, alisema iwapo mwanamchama huyo mpya atapitishwa kugombea ubunge itakuwa ni kupoka demokrasia na kanuni za chama.

“Hatupo tayari kuona anatuvuruga, kama alifanya huko, hatutakubali, taarifa hizi zinatuumiza sisi Monduli.

“Tunataka aje kwa wananchi, atuambie, huyu amekuja kwetu na afuate utaratibu kwa mujibu wa kanuni za chama,” alisema.
Akizungumzia madai hayo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Monduli, Wilson Lengima, alisema, hahusiki kumpigia debe Kalanga kuwa mgombea ubunge.

Hata hivyo, alisema aliwahi kusikia baadhi ya malaigwanani walikuwa na kikao hivi karibuni wakitaka Kalanga agombee ubunge.

Alisema kikao hicho hakikuwa cha chama na taratibu za kuwapata wagombea zitafuatwa kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama.
Alisema hadi sasa chama hakina mgombea ye yote na akawataka wanachama kuwa watulivu.


Kalanga Apingwa na Wananchi wa Monduli Kalanga Apingwa na Wananchi wa Monduli Reviewed by KUSAGANEWS on August 07, 2018 Rating: 5

No comments: