Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
William Ole Nasha ametoa wiki mbili kwa mkandarasi anayefanya ukarabati wa
majengo katika shule ya sekondari ya Mtwara Ufundi kuhakikisha anayakabidhi
Ametoa kauli hiyo jana Agosti 15, 2018 katika ziara yake ya
kikazi ya kukagua miundombinu ya shule
“Lazima waje ndani ya wiki mbili wakabidhi mradi na wasipofanya
hivyo hakutakuwa na muda wa kutazama na kueleza upungufu,” amesema
“Majengo yakishaanza kutumika itakuwa vigumu kujua
kama ni wao hawajafanya vizuri au kuna uharibifu umefanyika.”
Naibu waziri huyo pia alikutana na viongozi wa sekta ya
elimu na wakuu wa shule na kufanya nao mazungumzo
Katika mazungumzo hayo alielezwa siri ya Mkoa wa Mtwara
kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita, kuombwa yafanyike mabadiliko
ya utungaji wa mtihani wa darasa la saba.
Mwalimu Mkuu wa
sekondari ya Nangwanda, Beatrice Marwa ameshauri Serikali kubadili aina ya
mtihani wa kumaliza darasa la saba ili kubaini watoto wanaofaulu na kuanza
kidato cha kwanza wakiwa hawajui kusoma na kuandika
“Naomba kutoa ushauri kwa upande wa shule za msingi, mtihani
wa kuhitimu darasa la saba mfumo wake ubadilike turudishe wa zamani wa swali,
kazi na jibu,” amesema
“Kama ni hesabu ionekana anafanya hesabu na anaandika mwenye
jibu, hii itasaidia kubaini watoto wasiojua kusoma na kuandika kuliko hii ya
kuchagua mtoto anaweza akabahatisha na kufaulu. Akifika sekondari unagundua
hajiwezi katika kuandika.”
Ole Nasha ameahidi kulifanyia kazi wazo hilo kwani tayari
lipo na mipango imeshaanza.
Naibu waziri Wa Elimu atoa Wiki 2 Kwa Mkandarasi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment