Meneja masoko wa Kampuni ya Mabati ya ALAF Theresia
Mmasy ambao ndio wazamini mashindano yahoo akizungumza na wandishi wa habari
katika ukumbi wa Karimjee.
|
Na Christina Mwagala
Mwinyi Mgeni
rasmi mashindano ya mashairi ya Meya wa jiji la Dar.
RAIS Mstaafu
wa awamu ya pili ,Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
mashindano ya mashairi ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita
yatakaofanyika Septemba moja na mbili mwaka huu katika ukumbi wa Karimu
Jee.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini hapa leo, kwa niaba ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar
es Salaam, Mratibu wa mashindano hayo ,Shehe Mwita Kambi amesema kuwa lengo la
mashindano hayo ni kukuza lugha ya Kiswahili hapa nchini.
Amefafanua
kuwa washiriki wa mashindano hayo ni wakazi wa jijini hapa ambapo kila mmoja
atapaswa kutunga shairi lisilozidi beti nane na kupungua beti kumi.
Mashindano
hayo ya mashairi ambayo hufanyika kila mwaka ,hukusudia hukutanisha
magwiji,wakongwe wa lugha ya Kiswahili na hivyo washindi kupatiwa zawadi ya
fedha Tathilimu kwa mshindi wa kwanza hadi wa kumi bora.
“Lengo kubwa
la mashindano haya ni kukuza lugha ya Kiswahili, ambayo ndio Lugha Mama,
mtakubaliana na mimi kuwa viongozi wetu wa serikali ,akiwemo rais Dk. John
Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kutangaza lugha hii kwani wote ni
mashahidi kwamba hata katika ziara zake za nje ya nchi amekuwa akihutubia kwa
kutumia lugha ya Kiswahili” amesema Shehe Mwita.
Kutokana na
umuhimu wa tukio hilo” Niwakaribishe wananchi wa jijini hapa kujitokeza kwa
wingi kwenye mashindano hayo,mshindi wa kwanza atapatiwa fedha kiasi cha
shilingi milioni moja, wapili shilingi laki tano, watatu shilingi laki tatu,na
mshindi wan ne hadi wa kumi atapatiwa shilingi laki moja.
Aidha
mratibu huyo amesema kuwa ,ujumbe wa mwaka huu katika utungaji wa mashairi ni “LUGHA
YETU,FAHARI YETU, huku akitumia nafasi hiyo kuipongeza kampuni ya mabati ya
ALAF kwa kuzamini mashindano hayo.
Kwaupande wake
Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Theresia Mmasy amesema kuwa lengo la kuzaminishi
mashindano hayo ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na viongozi wa serikali
katika kuhakikisha kwamba wanatangaza lugha ya Kiswahili hapa nchini na nje ya
nchi.
Amefafanua
kuwa kila mwaka wamekuwa wakiendesha mashindano hayo na kwamba mwaka huu
wameona kuna tija ya kumuunga mkono Meya wa jiji la Da es Salaam kutokana na
kuonyesha nia ya kukuza lugha hiyo.
Mwinyi Mgeni rasmi mashindano ya mashairi ya Meya wa jiji la Dar.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment