Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule
ya Sekondari Old Tanga, Shufaa Mbughuni amekutwa amefariki dunia huku uso wake
ukiwa umechubuliwa ngozi.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga,
Edward Bukombe amesema mwili wa mwanafunzi huyo umekutwa jana Agosti 19, 2018
saa 9.40 alasiri katika mtaa wa Majani Mapana kata ya Nguvumali jijini Tanga.
Bukombe alisema taarifa kamili
kuhusiana na tukio hilo ataitoa mara baada ya madaktari wa hospitali ya
mkoa wa Tanga ya Bombo kuufanyia uchunguzi mwili wa mwanafunzi huyo.
Naye baba wa mwanafunzi huyo ambaye
pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Majani Mapana, Salim Mbughuni amesema
mwanaye aliwaaga wenzake juzi saa 2.00 usiku kwamba anakwenda kijisomea lakini
hakurudi kama ilivyo kawaida yake.
Mwanafunzi Kidato cha Nne Auawa Kikatili Tanga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment