Mvua ya upepo iliyonyesha jana Agosti 3, 2018 katika
kijiji cha Iteja Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza imesababisha hasara ya zaidi
ya Sh15 milioni
Mvua hiyo imeezua paa za nyumba kadhaa ikiwemo vyumba vya
madarasa katika shule sekondari Aimee Mirembe
Akizungumza leo Jumamosi Agosti 4, 2018 mkuu wa Wilaya ya
Misungwi, Juma Sweda amesema paa la madarasa mawili, vyoo vya wanafunzi na
ofisi ya walimu katika shule ya msingi Isuka iliyoko kata ya Kasololo wilayani
humo pia yameezuliwa
"Paa la nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Kwima
pia limeezuliwa," amesema Sweda
Ofisa elimu sekondari Wilaya ya Misungwi, Diana Kubofa
amesema hasara iliyosababishwa na mvua hizo ni zaidi ya Sh15 milioni
Akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama
iliyotembelea kijiji hicho kukagua madhala ya mvua, mkuu wa shule
ya sekondari Aimee Mirembe, Florencia Ndubashe amesema vyumba vinne vya
madarasa, ofisi ya walimu pamoja na vyumba viwili vya maabara vimeezuliwa paa
"Hii ni mara ya pili miundombinu ya majengo katika
shule yetu yanaathiriwa na mvua ya upepo. Mwaka 2013 mvua kubwa iliyoambatana
na upepo iliezua paa ya vyumba viwili vya madarasa," amesema Mwalimu
Ndubashe
Mkuu wa wilaya amesema mchakato wa kukarabati miundombinu
yote iliyoharibiwa imeanza kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo haraka
iwezekanavyo
Mvua iliyoezua mapaa yasababisha hasara ya Sh15 milioni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 04, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 04, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment